Maafa yatokea wilayan rungwe watu 5 wafariki dunia kati yao 3 ni familia moja.soma zaid.
Watu watano wamefariki dunia kati yao watatu
wakiwa wa familia moja baada ya nyumba
waliyokuwa wakiishi kufunikwa na udongo baada
ya mvua kubwa kunyesha kwa saa kumi wilayani
Rungwe.
Mvua kubwa ambayo imenyesha kwa zaidi ya
saa 10 mfululizo ndiyo ambayo imesababisha
udongo kuporomoka kutoka katika Mlima
Mkomelo na kusababisha madhara makubwa
ikiwemo vifo vya watu watano na uharibifu wa
mazao ya chakula na biashara katika kijiji cha
kitali,halmashauri ya busokelo wilayani rungwe
Kutokana na maporomoko hayo ya
udongo,familia ya Iman John Mwakyusa
imejikuta ikipoteza watoto watatu ambao ni
wanafunzi baada ya nyumba waliokuwa wakiishi
kufunikwa na udongo.
Mratibu wa Maafa katika Halmashauri ya
Busokelo Maombi John Msuta amesema maafa
hayo yametokana na mvua kubwa ambazo
zinanyesha kwenye eneo hilo na sasa
halmashauri yake imeanza kuchukua hatua za
tahadhari ikiwemo kuwahamisha watu wanaoishi
kwenye maeneo hatarishi.chanzo itv.
0 comments :
Post a Comment