Kama ulikuwa hujui leo ni siku ya kuzaliwa kwa rais mstaafu wa awamu ya pili mh.Ally hassan mwinyi.
Alipoingia madarakani kumpokea aliyekuwa Rais
wa Awamu ya kwanza, Mwalimu Julius Nyerere
mnamo tarehe 5 Novemba mwaka 1985,
watanzania wachache sana labda waliweza
kudhani kwamba miaka kumi baadaye na zaidi
baada ya kustaafu rasmi, ataibuka kuwa
mmojawapo wa marais wa Tanzania ambao
watabakia kupendwa na kuheshimika kwa namna
ya kipekee kabisa.
Mpaka anakabidhi madaraka yake ya urais kwa
rais wa awamu ya tatu, Ndugu Benjamin William
Mkapa mnamo tarehe 23 Novemba mwaka 1995,
jina ambalo wengi tulipenda kulitumia ni “Mzee
Rukhsa” ingawa kamwe hatukuwahi kusahau
kwamba jina lake kamili ni Ali Hassan Mwinyi,
Raisi wa awamu ya pili wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania.
Tarehe kama ya leo, Mei 8 1925, miaka 91
iliyopita, Ali Hassan Mwinyi alizaliwa katika kijiji
cha Kivure, wilayani Kisarawe, mkoa wa Pwani,
Katika nchi ya 'Tanganyika', akiwa bado mwenye
umri mdogo sana familia yake ilihamia Zanzibar.
Pichani ni Rais Mwinyi akiwa na aliyekuwa
Makamu wa Rais wa Kamisheni ya Ulaya (EC) -
Mahusiano, Maendeleo na Uvuvi, Ndugu Manuel
Marín Mjini Brussels Ubelgini wakati wa ziara ya
Rais Mwinyi huko. Picha ilipigwa April 12, 1991.
Picha Ni Kwa Hisani ya Hifadha ya Watanzania
Mashuhuri..
0 comments :
Post a Comment