Kiwango cha kuvunjika ndoa kimeendelea kushika kasi hizi ni takwimu.soma zaid.
Idadi ya talaka zilizosajiliwa na Wakala wa Usajili
wa Vizazi, Vifo, Talaka na Ndoa (Rita) kwa
mwaka 2013/14 ni 99; mwaka 2014/15 zilikuwa
talaka 150.
Dar es Salaam. Takwimu za kuvunjika kwa ndoa
zinaongezeka kwa kasi na sasa siyo kifo
kinachowatenganisha wapendanao, bali sheria
hulazimika kuchukua mkondo wake.
Idadi ya talaka zilizosajiliwa na Wakala wa Usajili
wa Vizazi, Vifo, Talaka na Ndoa (Rita) kwa
mwaka 2013/14 ni 99; mwaka 2014/15 zilikuwa
talaka 150.
Kwa mujibu wa Rita licha ya kuwa ndoa nyingi
zinavunjika, lakini hazivunjwi kisheria na talaka
zinazotolewa ni batili kwa sababu hazitambuliwi
na wakala huyo.
Meneja wa Mawasiliano, Taarifa na Elimu kwa
Umma wa Rita, Josephat Kimaro amesema
kuachana kienyeji au kupeana talaka
zisizotambuliwa na Rita kuna madhara lukuki,
ikiwamo kukosa mirathi, kushindwa kuoa au
kuolewa na kusababisha migogoro kwenye
familia.
0 comments :
Post a Comment