Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, June 30, 2016

Kocha wa timu ya taifa ya malawi amefutwa kazi ya ukocha.soma zaid.


Malawi imemfuta kocha wa timu ya taifa pamoja
na msaidizi wake.
Mikataba ya Ernest Mtawali na msaidizi wake
Nsanzurwimo Ramadahan, ilitarajiwa kumalizika
31 Julai.
Wawili hao wamefutwa baada ya Malawi
kuondolewa kutoka michuano ya Kombe la
Cosafa katika hatua ya makundi.
Mtawali, 49, aliyekuwa kiungo wa kati wakati wa
uchezaji wake, alichukua hatamu katika timu ya
taifa Agosti 2015.
Chini ya uongozi wake, timu hiyo ya taifa
ilishinda mechi sita, ikashindwa mechi sita na
kutoka sare mechi nne.
Ramadahan hata hivyo anatarajiwa kurejea kama
mkufunzi wa muda kuongoza Malawi dhidi ya
Swaziland mwezi Septemba.
Mechi hiyo, itakayochezwa tarehe 3 Septemba
mjini Blantyre, ndiyo ya mwisho kwa Malawi
baada ya kushindwa kufuzu kwa michuano ya
Kombe la Taifa Bingwa Afrika 2017.
Matumaini ya Malawi kufuzu kwa michuano hiyo
itakayoandaliwa nchini Gabon mwaka ujao mwezi
Juni baada yao kulazwa na Zimbabwe mjini
Harare. Malawi wanashika mkia Kundi L wakiwa
na alama mbili.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top