Roli la mizigo limesababisha taharuki baada kuanguka bila dereva huko Ruvuma.soma zaid.
Watu watano wamenusurika kufa wilayani
Songea mkoani Ruvuma baada ya roli
lililoegeshwa kuporomoka bila dereva na
kugonga maduka na nguzo za umeme na
kusababisha taharuki kubwa na kujeruhi
watu wawili waliolazwa katika hospitali ya
mkoa wa Ruvuma huku shughuli
zikisimama na barabara ya Songea-
Mbinga kulikotokea ajali ikifungwa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
wanaelezea jinsi tukio lilivyotokea na
namna roli hilo lililoporomka bila dereva
na kuparamia maduka na kugonga nguzo
za umeme mjini Songea na kujeruhi watu
wawili na kugonga kwenye duka la vifaa
vya umeme la Bw. Henry Tweve
aliyekuwemo ndani ya duka hilo na watu
wengine wawili ambapo pia limejeruhi
watu wengine wawili kabla ya kugonga
duka hilo.
[IMG]
Baadhi ya wananchi wamelaani kitendo
cha kuegesha maroli mjini wakatiu
serikali ilipiga marufuku maroli
kuegeshwa mjini na kuitaka serikali
kusimamia sheria zake ilizojiwekea za
kuhakikisha maroli hayaegeshwi mjini ili
kuepesha ajali kama hizo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma
Bw. Zuberi Mwombeji alipopigiwa simu
yake ya mkononi ilipokelewa na mlinzi
wake aliyesema yuko msibani huku
waathirika wa ajali hiyo wakieleza hasara
walizozipata.
Chanzo: ITV
0 comments :
Post a Comment