Watu 200 waliokimbia Boko Haram wamefariki Dunia.soma zaid.
Watu 200 waliokimbia kutoka kwa maeneo
yaliyovamiwa na wanamgambo wa kiislamu wa
Boko Haram nchini Nigeria, wamefariki kutokana
na baa la njaa na ukosefu wa maji.
Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka- MSF,
linasema kuwa vifo hivyo viltokea mwezi uliopita,
katika kambi moja duni ya wakimbizi wa ndani
kwa ndani, Kaskazini- Mashariki mwa nchi hiyo.
MSF linasema kuwa uhaba huo wa vyakula na
maji unatishia maisha ya wakimbizi zaidi wa
ndani kwa ndani katika kambi ya wakimbizi ya
Bama Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Kambi hiyo yamkini inawakimbizi takriban elfu
20,000 hivi.
MSF inasema kuwa mmoja kati ya watoto
watano katika kambi hiyo wanaugua utapiamlo.
Umoja wa mataifa unakisia kuwa machafuko
yaliyosababishwa na wanamgambo wa Boko
Haram maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa
Nigeria yamesababisha watu milioni 2 kutoroka
makwao.
0 comments :
Post a Comment