Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, June 9, 2016

Zahanati wilayani mvomero haijanza kutumika zaid ya miaka 17 mpaka sasa.

Zahanati ya Kata ya Nyandira wilayani
Mvomero haijaanza kutumika tangu
ijengwe zaidi ya miaka 17 iliyopita kwa
kukosa vifaa tiba na wauguzi huku
wananchi wakitembea umbali mrefu
kutafuta huduma za afya.
Diwani wa kata hiyo alisema kuwa
ukosefu huo unawatesa wananchi kwani
hulazimika kufuata huduma za afya mbali
na vijiji vyao hivyo kupelekea vifo vya
wajawazito na watoto. Wananchi hao
hulazimika kwenda kupata huduma katika
kituo cha Afya cha Langali ambacho kipo
umbali wa kilomita tano kutoka Nyandira.
Diwani huyo aliitaka serikali kupitia wizara
husika kuharakisha uletaji wa vifaa
pamoja na watumishi hao kwani ni jambo
la ajabu wananchi kuteseka kwa kukosa
huduma ya afya huku zahanati walioijenga
kwa nguvu zao ikikaa bila kutumika.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top