Maafisa 302 wa polisi nchini kenya wasimamishwa kazi.soma zaid.
Takriban maafisa 302 wa polisi wamefutwa kazi
nchini Kenya kwa kukataa kukaguliwa tangu
mpango huo wa kutaka kukabiliana na ufisadi
kuanzishwa mwaka 2013,kulingana na tume
inayotekeleza ukaguzi huo.
Hayo yalibainishwa na Jonhston Kavuludi
,anayeongoza tume hiyo ya huduma za maafisa
wa polisi huku maafisa wa polisi wakijiandaa
kuhojiwa na jopo katika mji wa magharibi wa
Kisumu.
Ukaguzi huo ni mpango wa uma na hufanywa
mbele ya kamera ambapo maafisa uhojiwa
kuhusu mali na fedha wanazomiliki huku
mgongano wowote wa maslahi ukichunguzwa.
Mwezi uliopita wakati jopo hilo lilipokuwa
Mombasa ,afisa mmoja wa idara ya trafiki
hakuweza kusema ni wapi alipata takriban dola
500,000 ambazo ziliwekwa katika mtandao wa
simu unaotuma fedha ama kupokea na akaunti
yake ya benki.
Wakenya katika mitandao ya kijamii
walishangazwa na kuelezea vile
wanavyolazimishwa kutoa hongo baada ya
kukamatwa kwa makosa ya trafiki.chanzo BBC swahik
0 comments :
Post a Comment