Herry kitily na mwenzake shose sinare sasa kujibu shitaka la nne la utakatishaji wa fedha.soma zaid.
Mkurugenzi wa mashtaka ‘DPP’ alikata Rufaa
mahakama kuu ya Tanzania akipinga uamuzi wa
kufutwa kwa shtaka la nane la utakatishaji fedha,
uamuzi uliotolewa na Mahakama ya hakimu
mkazi Kisutu na hakimu mkazi Emillius Mchauru
kwenye kesi inayowakabili Kamishna Mkuu wa
zamani wa TRA Harry Kitilya, aliyekuwa Miss
Tanzania mwaka 1996 , Shose Sinare na
mwanasheria wa Benki ya Stanbic, Sioi Solomon.
June 09 2016 Mahakama ya Rufani imetengua
uamuzi wa Mahakama Kuu Tanzania kanda ya
Dar es salaam iliyotupilia mbali rufaa ya
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ya kupinga
kufutwa kwa shtaka la nane la utakatishaji fedha
katika kesi inayomkabili aliyekuwa Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Harry Kitilya na wenzake wawili.
Hukumu hiyo imesomwa leo mahakamani hapo
na Msajili wa mahakama hiyo, Zahra Maluma
ambapo alisema mbali ya kutenguliwa kwa
uamuzi huo pia Mahakama Kuu imeamriwa
kusikiliza rufani ya msingi ya DPP.
Msajili Maluma alibainisha kuwa hatua hiyo
inatokana na jopo la majaji kupitia uamuzi wa
Mahakama Kuu na kubaini kwamba Jaji Moses
Mzuna alikosea kutoa uamuzi uliosema kuwa
kufutwa kwa shtaka la nane la utakatishaji fedha
katika kesi inayomkabili Kitilya na wenzake
hakutamaliza wala kuathiri shauri hilo.
0 comments :
Post a Comment