Waziri mkuu Narendra Modi ahutubia bunge la marekani.soma zaid.
Waziri mkuu wa India Narendra Modi akihutubia
bunge la Marekani
Shirikisha
Kama kiongozi wa taifa liillokumbwa na
migawanyiko ya madhehebu, kidini na kikabila,
waziri mkuu wa India Narendra Modi anatafuta
uwelewano na wabunge wa marekani kwa
kutumia ucheshi.
Bw Modi aliwaambia wabunge wa Marekani kuwa
nimeambiwa kazi ndani ya bunnge zinafanyika
kwa Amani. Anasema pia nimeambiwa kuwa
mnajulikana sana kwa ushirikiano baina ya vyama
vyenu. Bw Modi alipigiwa makofi ikifuatiwa na
vicheko baada ya kutoa kauli hiyo, pale
alipokutana na wabunge wa Marekani jana
Jumatano.
Bw Modi aliendelea kuwaambia wabunge hao
kuwa hawako peke yao. Alisema, mara kwa mara
yeye pia hushuhudia hali kama hiyo katika bunge
la India. Kwa hivyo tuna mifano mingi ya pamoja.
Bw Modi alisema kushamiri kwa ushirikiano wa
biashara na nishati, na hata maslahi ya
kimkakati, na kuongezea kuwa umbali na hali ya
kutokuaminiana amabyo awali iliashiria uhusiano
wa India na Marekani, sasa ni jambo la zamani.
Anasema uhusiano wetu umevuka kusitasita za
historia, na sasa ukweli na muunganiko
unafafanua majadiliano yetu, na bw Modi alisihi
kuwepo na ushirikiano wa karibu zaidi kwa
malengo yao pamoja.
Hotuba ya Modi ilikuwa ni ya tano kuwahi
kutolewa na mkuu wa serikali ya India kwa bunge
la marekani. Hotuba hio inafwatia mkutano wa
jumanne na rais Barack Obama na tangazo kuwa
India itajenga vinu 6 vya nyuklia vitakavyojengwa
na makampuni ya Marekani, hiyo ikiwa matokeo
ya makubaliano ya kiraia ya kinyuklia kati ya
mataifa hayo mawili ambayo yalifikiwa mwaka
2008.
0 comments :
Post a Comment