Zeshi la polisi zanzibar inaongoza kwa kuomba rushwa.soma zaid.
Mkuu wa Elimu kwa Umma wa Mamlaka hiyo,
Shuweha Abdalla Omar alisema jana kuwa jeshi
hilo linaongoza kwa kuomba na kupokea rushwa
kwa asilimia 50, wakati Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) visiwani humo ikiwa na asilimia
37 na mahakama ikiwa na asilimia 36.
By Masanja Mabula, Mwananchi, mmasanja@
mwananchi.co.tz
Zanzibar. Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia
Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar
(Zaeca), imesema Jeshi la Polisi visiwani humo
linaongoza kwa vitendo vya rushwa ukilinganisha
na taasisi nyingine.
Mkuu wa Elimu kwa Umma wa Mamlaka hiyo,
Shuweha Abdalla Omar alisema jana kuwa jeshi
hilo linaongoza kwa kuomba na kupokea rushwa
kwa asilimia 50, wakati Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) visiwani humo ikiwa na asilimia
37 na mahakama ikiwa na asilimia 36.
Akizungumza na Polisi Mkoa wa Kaskazini
Pemba, Shuweha alisema utafiti uliofanywa na
Afro Barometer kwa kushirikiana na Repoa katika
kipindi cha mwaka 2014, ulibaini kiwango hicho
cha rushwa kwa taasisi hizo.
Alisema Zaeca tayari imepokea tuhuma 10
zinazowahusu baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi
waliotuhumiwa na kuhusika na vitendo vya
rushwa na kusisitiza kwamba, upelelezi
ukikamilika watafikishwa mahakamani.
“Askari wa kikosi cha usalama barabarani
wanapokamata gari lenye makosa badala ya
kuchukua hatua na kumuelimisha mkosaji ili
wakati asirudie makosa, humtoza kiwango kidogo
cha fedha na kujipatia maslahi yao binafsi,”
alisema.
Shuweha alitoa rai kwa askari hao kufanya kazi
zao kwa welei na kwa kuzingatia maadili ili
kuepuka kashfa hiyo.
Mwanasheria wa Zaeca, Abubakar Mohammed
alisema taasisi hiyo haitamuonea huruma askari
yeyote atakayebainika kuhusika na vitendo vya
rushwa. Pia, aliwaomba viongozi wa juu wa jeshi
hilo kushirikiana na mamlaka zingine kuhakikisha
wanaotuhumiwa wanawajibishwa kwa mujibu wa
sheria za jeshi hilo ili kulinda heshima na hadhi
jeshi.
Msaidizi wa Kamanda wa Polisi Pemba, Mlenge
Mohammed Mlenge, aliwataka watendaji wa
mamlaka hiyo kuwasiliana na Polisi mara
wanapopokea tuhuma zinazowahusu askari ili
wachukue hatua za kinidhamu.chanzo mwananch.
0 comments :
Post a Comment