Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, June 9, 2016

Moshi# Raia wa Tego ahukumiwa maisha kwende jela.soma zaid.


Moshi. Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya
Moshi imemhukumu kifungo cha maisha gerezani
raia wa Togo, Josiane Dede (25) kwa kosa la
kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine
zenye thamani ya Sh116 milioni.
Akitoa hukumu hiyo jana, Jaji wa Mahakama
hiyo, Benedict Mwingwa alisema imeridhika na
ushahidi uliotolewa na mashahidi tisa wa upande
wa mashtaka.
Alisema kutokana na ushahidi huo, Mahakama
inamtia hatiani mshtakiwa huyo kwa kosa la
kusafirisha dawa hizo zenye uzito wa gramu
1,989 kinyume cha Sheria namba 6 kifungu cha
31 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012.
Jaji Mwingwa alisema mwaka 2013, mshtakiwa
huyo alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Kilimanjaro (Kia) akiwa na mabegi mawili,
moja likiwa na dawa hizo.
Akitoa utetezi kabla ya hukumu kutolewa, wakili
wake, David Shiratu alidai kuwa mteja wake
anaiomba Mahakama kumpunguzia adhabu kwa
sababu ni mwanafunzi wa utalii katika Chuo
Kikuu cha Togo na familia yake pamoja na nchi
yake inamtegemea.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top