Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, June 9, 2016

Al-shabab yasababisha taharuki kambi ya wanajeshi wa Ethiopia.soma zaid.

Al-Shabab wavamia kambi ya wanajeshi wa
Ethiopia
Wapiganaji wa kundi la al-Shabab nchini Somalia
wanasema kuwa wamewaua wanajeshi 40 wa
Ethiopia katika kambi ya Umoja wa Afrika katikati
ya Somalia.
Wakaazi wa Halgan wameiambia BBC kwamba
walisikia mlipuko mkubwa uliofuatiwa na
ufyatulianaji wa risasi.
Umoja wa Afrika Amisom umethibitisha kuhusu
shambulio hilo lakini unasema lilikabiliwa vilivyo.
Amisom inaunga mkono serikali ya Somalia huku
ikitafuta kulidhibiti taifa hilo kutoka kwa mikono
ya wapiganaji wa al-Shabab.
Katika misururu ya ujumbe wa Tweeter Amisom
imesema kuwa wanajeshi wake wakisaidiwa na
wale wa Somalia waliwafurusha washambuliaji
hao ambao sasa wametoroka huku wakisakwa na
wanajeshi wa Amisom.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top