BAVICHA wamsaliti Freeman mbowe kuhusu kwenda Dodoma.soma zaid.
BARAZA la vijana la Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), limeapa kwenda mkoani
Dodoma kusaidia jeshi la polisi kuzuia mkutano
mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Anaandika Josephat Isango… (endelea).
Kiongozi mmoja mwandamizi wa BAVICHA
makao makuu aliyezungumza na MwanaHALISI
Online kwa sharti la kutotajwa jina lake
amesema, uamuzi wa wao kwenda Dodoma uko
palepale.
❝
“Tumeshaamua kwenda Dodoma na hakuna
yeyote anayeweza wa kutuzuia. Uamuzi wetu
uko palepale na tutatekeleza kila ambacho
tumepanga,” ameeleza.
Mkutano mkuu wa CCM umepangwa kufanyika
mkoani Dodoma wiki mbili zijazo. Unatarajiwa
kumchagua John Pombe Magufuli, kuwa
mwenyekiti wa taifa wa chama hicho.
Msimamo mkali wa kiongozi huyo wa BAVICHA
umefuatia uamuzi wa mwenyekiti wa taifa wa
chama hicho, Freeman Mbowe, kuzuia vijana wa
Chadema kwenda Dodoma kukabiliana na CCM.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana Jumapili, kufuatia
kuwapo kwa taarifa kuwa jeshi la polisi nchini,
limeapa kupambana na viongozi na wafuasi wa
Chadema, ikiwa watafika mkoani humo kuzuia
mkutano wa CCM.
Chadema kimeamua kuchukua hatua ya
kukabiliana na CCM baada ya jeshi la polisi
kuzuia mikutano ya ndani ya chama hicho;
mikutano ya hadhara na mahafali yaliyopangwa
kufanywa na Umoja wa Wanavyuo wa Chadema
(CHASO), katika baadhi ya mikoa.
Kauli ya Mbowe imepingwa na baadhi ya vijana
katika maeneo mbalimbali, ikiwamo mkoani
Arusha, ambako uongozi wa mkoa umekabidhi
kwa BAVICHA kiasi cha Sh. 5 milioni kwa ajili ya
kwenda Dodoma.
Miongoni mwa mahafali ya Chadema
yaliyovurumishwa na polisi, ni pamoja na yale
yaliyofanyika mkoani Dodoma ambako mgeni
rasmi alikuwa waziri mkuu mstaafu, Frederick
Sumaye.
Mahafali ya Dodoma yalitarajiwa kufanyika katika
hoteli ya African Dreems, yaliporomoshwa na
polisi kwa kutumia mabomu ya machozi, silaha
za moto na gari moja la maji ya kuwasha.
“Upole wa Mbowe na Edward Lowassa, ndiyo
uliosababisha tukaibiwa kura na kushindwa
kuandamana. Katika hili, hatuko tayari kumsikiliza
yeyote,” ameeleza kiongozi huyo.
Anasema, “…kama Mbowe ameshindwa kuongoza
chama basi ni vema akaamua kukaa pembeni na
kuwacha wenye uwezo na ujasiri wa kutenda.
“Kama anaogopa kuwekwa ndani basi aache
kabisa siasa hadi watakapopatikana polisi wapole
atarudi kuwa mwenyekiti.”
Akiongea kwa uchungu kiongozi huyo
mwandamizi wa Chadema anasema, “tunataka
kwenda Dodoma ili azima yetu itimie. Ni lazima
polisi na CCM wafahamu kuwa nchi hii siyo mali
ya genge la watu wachache. Nasi ni umma
ambao unapaswa kutendewa haki.”
Katika mitandao ya kijamii kumesheheni mijadala
inayopinga kauli na msimamo wa Mbowe wa
kuwazuia BAVICHA kwenda Dodoma na wengine
kufikia hatua ya kumshambulia.
Baadhi ya waliojitokeza kupinga uamuzi huo wa
Mbowe, ni viongozi wenzake wa Kamati Kuu (CC)
, Baraza Kuu la taifa (BKT), wabunge, madiwani
na viongozi wa mikoa.
Hatua ya polisi kuzuia mikutano ya hadhara
ilifuatia kauli ya Magufuli, aliyotangaza zuio la
jumla la kufanyika mikutano ya kisiasa ya
hadhara na ya ndani na kusema, “wanaotaka
kufanya siasa wasubiri hadi mwaka 2020.”chanzo mwanahalisi online.
0 comments :
Post a Comment