Breaking News
Loading...

Advert

Friday, July 29, 2016

Ratiba ya Treni kuelekea kigoma na mwanza zabadilika.soma zaid.

Kampuni ya Reli ya Tanzania (TRL)
imefanya mabadiliko ya muda wa Treni ya
Abiria kulekea mikoa ya Kigoma na
Mwanza ambapo kuanzia tarehe 02 Agosti
2016 Treni itaanza kuondoka saa tisa(9)
mchana badala ya saa 11 jioni muda wa
sasa.
Mabadiliko hayo yametangazwa na
Meneja Uhusiano wa TRL Midladjy Maez
wakati akizungumza na waandishi wa
habari Ofisi kwake leo Jijini Dar es
Salaam.
Maez amesema kuwa mabadiliko hayo
yamefanyika ili kutoa nafasi kwa treni ya
pili ya huduma za Jiji kutoka kituo Kikuu
cha Reli cha Dar es Salaam kwenda Pugu
ambayo itaanza kutoa huduma mapema
siku ya Jumatatu ya tarehe 01/08/2016.
Aliongeza kuwa mabadiliko hayo
yanahusu treni za abiria za huduma za
kawaida zinazoondoka siku za Jumanne na
Ijuma na kubainisha kuwa kwa upande wa
huduma za treni ya Deluxe zitaendelea na
muda wake wa kawaida.
“Uongozi umeamua kufanya mabadiliko
haya kwa sababu za kiusalama zaidi
kwani mabadiliko haya yataepusha
muingiliano unaoweza kupelekea ajali na
kuongeza kuwa kwa safari za kutoka
Kigoma na Mwanza muda umebaki
uleule”. Alisema Maez.
Meneja Uhusiano huyo aliongeza kuwa
huduma za treni ya Jiji kwenda Pugu
itakuwa na vituo 10 ambavyoa alivitaja
kuwa ni pamoja na Pugu Stesheni, Gongo
la Mboto,FFU Mombasa, Banana, (njia
panda kwenda Stesheni), na karakata.
Vingine ni pamoja na Vingunguti Mbuzi,SS
Bhakressa, Kamata na Kituo Kikuu cha
reli Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa huduma hiyo itakuwa na
awamu mbili asubuhi na Alasiri ambapo
treni ya kwanza itaondoka kituo cha Pugu
saa 12 asubuhi na kuwasili kituo cha Dar
es Salaam sa 12:55 asubuhi na kufanya
safari tatu zitakazomalizika saa 05:15
asubuhi.
Jioni kutakuwa na safari tatu ambapo
treni itaondoka kituo cha Dar es Salaam
saa 09:55 alasiri kwenda Pugu na kuwasili
saa 10:50 jioni na safari ya mwisho kutoka
Pugu kuja Kituo Kikuu cha Dar es Salaam
saa 03:20 usiku.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top