Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, July 13, 2016

Uhakiki vyuo vikuu wanafunzi 2739 waingia mitini.soma zaid.

Dar es Salaam. Wanafunzi 2,739 mbalimbali
hawakujitokeza kuhakikiwa wakati Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
ilipofanya shughuli hiyo katika vyuo 26 nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa bodi hiyo, Jerry Sabi
amesema taarifa hiyo ni ya awali baada ya
uchambuzi taarifa za uhakiki wa vyuo 18 kati ya
26 vilivyohakikiwa.
Amesema bodi hiyo imetoa siku saba kuanzia leo
kwa wanafunzi ambao hawajahakikiwa kujitokeza
ili wahakikiwe vinginevyo wataonekana kuwa ni
wanafunzi hewa.
Amesema Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
ndicho kinachoongoza kuwa na wanafunzi wengi
wasiohakikiwa wanaofikia 763.
"Tunatoa muda wa ziada ili wanafunzi ambao
hawakupata nafasi ya kuhakikiwa kufanya hivyo
vinginevyo tutafuta mikopo yao," amesema.
Amesema orodha ya wanafunzi wasiohakikiwa
iko kwenye anuani ya mtandao wa bodi hiyo
ambayo ni www.heslb.go.tz.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top