Mahakama yatoa ufafanuzi wa taarifa iliyopotosha jamii.soma zaid.
Mahakama ya Tanzania inapenda kutoa
ufafanuzi kwa umma juu ya habari
iliyoandikwa na gazeti la kila siku la
Mwananchi toleo la Jumanne, Julai 12,
2016. Gazeti hilo lilichapisha habari
ambayo Mwandishi wa habari hiyo
alimnukuu Msajili Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania Mheshimiwa Katarina Revokati
akiwataka watendaji wa mahakama nchini
kujenga utamaduni wa kuwajibika na
kutoruhusu uhuru wa mahakama
kuingiliwa na watu kutoka nje ya
Mahakama.
Kutokana na habari hiyo, Mahakama ya
Tanzania inakanusha taarifa hiyo kwa
kuwa ililenga katika kuipotosha jamii na
kuleta msuguano kati ya Mahakama na
Taasisi nyingine.
UFAFANUZI WA TAARIFA HIYO
Mahakama ya Tanzania inapenda kutoa
ufafanuzi wa alichokisema Msajili Mkuu
wa Mahakama ya Tanzania wakati wa
ufunguzi wa Mkutano kuhusu Mpango
Mkakati wa Mahakama ya Tanzania
Jumatatu Julai 11, 2016 mjini Dodoma.
Aidha, Msajili aliwataka watumishi wa
mahakama nchini kutekeleza mpango
mkakati kwa nia thabiti na siyo kuutumia
uhuru wa mahakama vibaya kufunika
maovu, badala yake aliwataka wale wenye
kasoro katika utendaji wa kazi
kujirekebisha wao wenyewe ndani ya
mahakama la sivyo watarekebishwa hata
kutokea nje kwani jamii yetu kwa sasa
imedhamiria kubadilika na haitavumilia
utendaji mbovu kwa kigezo cha uhuru wa
mahakama.
Mahakama ya Tanzania inapenda
kuujulisha umma kuwa inafanya kazi na
watu wote na wadau wote nchini ili
kuhakikisha nchi inaenda inavyotakiwa na
haitaogopa kukosolewa kinyume na picha
iliyopelekwa kwa jamii na habari
iliyopotoshwa kwenye gazeti la
Mwananchi.
Mahakama inashauri waandishi wa
habari kuwasiliana na Mahakama endapo
kuna jambo lolote linalohitaji ufafanuzi.
Makosa mengine katika taarifa ni kama
vile kukosea cheo kwa kusema Jaji badala
ya Msajili Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania na kuandika taarifa kuhusu
hatua zinazochuliwa kwa Wahe. Majaji
waliohusika na sakata la ESCEOW ambapo
kiukweli katika mkutano huu
halikuongelewa kabisa.
IMETOLEWA NA KI TENGO CHA HABARI,
ELIMU NA MAWASILIANO.chanzo michuzi blog
0 comments :
Post a Comment