Bodi ya mikopo imetoa tahadhari kwa waombaji wa mikopo dhidi ya matapeli ambao sio watumushi .soma zaid
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya
Juu inapenda kuwatahadharisha
waombaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa
mwaka wa masomo 2016/2017 na umma
kwa imepokea taarifa kuwa kuna watu
wasio waaminifu ambao si watumishi wa
Bodi huwapigia simu baadhi ya waombaji
kwa lengo la kuwatapeli.
Taarifa hizo za kitapeli zimekuwa
zikisambazwa katika siku za hivi karibuni
kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii
zikiwataka baadhi ya waombaji wa
mikopo au wadhamini wao kutuma fedha
(Tshs 39,000/-) kwa namba ya simu
0716463190 ili fomu zao za maombi ya
mikopo zilizowasilishwa Bodi zirekebishwe
kwa kuwa zimeonekana zina makosa na
hivyo hawatapata mikopo.
Namba inayotumika kusambaza taarifa
hiyo au kupiga simu kutoa taarifa hizo ni
0764640325 na mtu anayepiga
anajitambulisha kwa jina la Charles Amos.
Bodi ya Mikopo inapenda kuwataarifu
wadau wake wote, wakiwemo wale
walioomba mikopo ya elimu ya juu kwa
mwaka wa masomo 2016/2017 kuwa
taarifa hizo si za kweli. Mtu huyo ni tapeli
na si mtumishi wa Bodi ya Mikopo.
Iwapo waombaji watapigiwa simu na
matapeli hao, watoe taarifa kwa vyombo
vya dola kwa hatua zaidi.
Aidha, Bodi ya Mikopo inapenda
kuwataarifu waombaji wa mikopo kuwa
utaratibu wa Bodi kuwasiliana na
waombaji wa mikopo ambao fomu zao za
maombi hubainika kuwa na upungufu
haujabadilika. Mara baada ya kazi ya
ukaguzi wa fomu kukamilika, Bodi ya
Mikopo itatoa taarifa kupitia vyombo
mbalimbali vya habari, ikiwemo tovuti
yake (www.heslb.go.tz) na kuwaalika
waombaji kufanya marekebisho.
Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti
ya Bodi iliyotajwa hapo juu.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA
MAWASILIANO,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA
ELIMU YA JUU,
IJUMAA, AGOSTI 12, 2016
0 comments :
Post a Comment