Wamachinga Dar kuendelea kuwepo maeneo yao ya kuuzia biashara waliyopangiwa.soma zaid.
RAIS John Magufuli ameutaka uongozi wa Jiji
na Manispaa za Dar es Salaam kutowaondoa
wafanyabiashara ndogo ‘machinga’ katika
maeneo waliyopo hadi watakapowatengenezea
utaratibu mzuri wa kufanya biashara zao.
Akizungumza na wanachama na wananchi
waliojitokeza kumpokea wakati alipofika katika
Ofisi Ndogo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam kwa ajili ya
kuingia kwenye ofisi yake ya uenyekiti kwa
mara ya kwanza, Rais Magufuli alisema umefika
wakati watu wanatakiwa kubadilika.
Alisema wamejipanga kufanya kazi kwa niaba
ya masikini kwa kuwa yeye hakuchaguliwa na
matajiri, hivyo atasimama kwa ajili ya masikini
kwa kuwa hata yeye ni mtoto wa masikini hivyo
atatembea na masikini wenzake, alisema
matajiri walipe kodi na masikini wasilipe kodi.
“Ninataka Dar es Salaam mpya, kwa hiyo hatua
nyingine tunazozichukua wapo wengine
wachache sana wanaweza wasizifurahie,
naomba muwapuuze kwa sababu tunafanya kwa
maslahi ya watu wa kawaida,” alisema.
Aliwataka viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam
waanze kujipanga namna watakavyotengeneza
mazingira mazuri kwa watu hao kufanya
biashara zao. Alitoa mfano kuwa, haiingii akilini
mtu kumtuma mgambo kwenda kumnyang’anya
mama lishe chakula chake, jambo ambalo
alisema ni dhambi kubwa.
Alisema anataka Tanzania ambayo masikini
anakuwa na haki sawa na tajiri, huku akiwataka
wafanyabiashara ndogo na wao kuzingatia
sheria, kwani hawawezi kujipanga katika eneo
moja.
Alisema kama watakuwa na vikundi vyao,
wakajipanga vizuri watauza ili mradi wanaweka
mazingira safi na si wanatengenezewa sehemu
nzuri na wao waigeuze genge la vibaka na hata
kufanya wateja wahofie kwenda.
Aidha, alisema kuna mchezo ambao unafanyika
kwa wafanyabiashara hao kwenda kuchukua
bidhaa kwa wauzaji wa bidhaa hizo na kuziuza
mitaani na kumfanya mtu huyo kukwepa kodi
wakati serikali inataka kukusanya kodi, hivyo ni
muhimu wanaponunua bidhaa zao wakumbuke
kudai kodi.
“Tunataka Dar es Salaam liwe jiji la biashara na
ndio maana sisi tumeamua kwenda Dodoma,
tunataka hapa pafanyike biashara za kimataifa,
hivyo wenye kuweza kufanya wafanye. Ndio
maana mimi na chama changu tuliamua
kupeleka muswada wa kuifanya nchi yetu kuwa
ya viwanda,” alisema Rais Magufuli.
0 comments :
Post a Comment