DaVID Kafulila ameibuka na kusema haya kuhusu uchumi wa tanzania katka kipindi hiki.soma zaid
DAVID Kafulila, aliyekuwa Mbunge wa jimbo la
Kigoma Kusini (2010-2015) amesema takwimu za
kiuchumi zinaonyesha hali ya Tanzania
inaendelea kuwa mbaya zaidi chini ya Serikali ya
awamu ya tano, anaandika Pendo Omary.
❝
Kafulila ambaye alipoteza ubunge katika
mazingira ya kutatanisha katika uchaguzi
Mkuu wa mwaka jana ameyasema hayo leo
jijini Dar es Salaam katika kongamano
lililoandaliwa na Baraza la Vijana wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) ili
kuadhimisha siku ya vijana duniani.
Kafulila amesema kuwa kwa sasa Tanzania ndiyo
nchi inayoongoza kwa deni kubwa Afrika
Mashariki ambapo deni la taifa la Tanzania ni
40% ya pato la taifa hali inayoliweka taifa pabaya
zaidi kiuchumi.
“Wakati hali ikiwa hivyo kwetu, deni la taifa la
Kenya ni 25% ya pato la taifa lao na deni la taifa
la Uganda ni 20 ya pato la taifa na bado Rais
John Magufuli anaendelea kukopa kwa kasi ya
ajabu,” amesema na kufafanua zaidi kuwa;
“Kwa mujibu wa ripoti ya robo mwaka ya Benki
ya Dunia katika kipindi cha robo mwaka tu cha
utawala wa Rais Magufuli tayari serikali yake
imekopa zaidi ya 900 milioni dola za kimarekani
ambazo ni zaidi ya Sh. 2 trilioni za kitanzania.”
Kafulila ametahadharisha kuwa kwa kasi ya
ukopaji ya Rais Magufuli na serikali yake suala la
serikali kujiendesha yenyewe kwa kujitegemea ni
ndoto ambayo haiwezi kufikiwa katika miaka ya
hivi karibuni.
“Wakati makusanyo yote ya mapato ya serikali
hapa nchini kwa mwezi ni 1.2 trilioni, malipo ya
mishahara peke yake ni zaidi ya 570 bilioni kila
mwezi lakini wakati huo huo serikali ya Tanzania
inalipa deni la Shilingi 500 bilioni kila mwezi.
Ameeleza.
Kafulila pia amesema licha ya tambo za serikali
ya Tanzania kuwa imeongeza ukusanyaji wa
mapato lakini fedha katika shughuli za msingi
zinazochochea ukuaji wa uchumi kama kilimo
zinazidi kufyekwa na serikali.
Ametoa mfano kuwa; Katika sekta ya kilimo
Mwaka 2015 serikali ilitoa 78 bilioni kama ruzuku
katika mbolea lakini mwaka huu serikali imetoa
10 bilioni tu kama ruzuku katika mbolea.
Lakini pia akisema mwaka jana akiba ya taifa ya
chakula ilikuwa zaidi ya tani laki 4 (400,000)
lakini mwaka huu akiba ya chakula ni tani elfu
sitini na nane pekee (68,000) na wakati huo huo
riba katika mikopo ya benki imepanda kutoka 14%
ya 2005 hadi 25% kwa mwaka 2015.
Kongamano hilo lenye mada, “kupiga vita
umasikini ili kufanikisha uzalishaji na matumizi
endelevu” linaendelea muda huu.chanzo mwanahalisonline
0 comments :
Post a Comment