Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, August 10, 2016

Freeman mbowe amewataka viongoi na wafuasi wa chama hicho kutotishika na vitisho vya polisi.soma zaid

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe,
amewataka viongozi na wafusi wa chama hicho
katika ngazi mbalimbali, kutotishika na vitisho
vya jeshi la polisi, anaandika Josephat Isango.

Mbowe amewataka wapenzi wa chama hicho
wakae mguu sawa kutekeleza maagizo ya
Kamati Kuu (CC), iliyoketi jijini Dar es Salaam
na kwamba wasitishwe na vitisho vya polisi.
Akizungumza na MwanaHALISI online Mbowe
amesema “Kama polisi wataendelea kuniita
sababu ya maazimio ya Kamati Kuu niliyosoma
mbele ya waandishi wa habari basi wananchi
waendelee na maandalizi sababu polisi
wamekuwa wakifanya siasa badala ya weledi wa
kazi yao.”
18 Septemba mwaka 2014 waliniita baada ya
kutangaza maandamano nchi nzima, wakanihoji
hawakunikuta na hatia wakaniacha hadi leo
hawajawahi kuniita, wanachofanya ni
kutupotezea muda wa kufanya siasa kwa mujibu
wa sheria, na hilo halikubaliki, aliongeza Mbowe.
2014 Mbowe akiwakilisha Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) alitangaza maandamano nchi
nzima. Kauli hiyo ilisababisha jeshi hilo kumwita
Mbowe makao makuu na kisha kumhoji.
Alikuwa akimtaka Rais Jakaya Kikwete kusitisha
Bunge Maalumu la Katiba kuendelea kwani
ilikuwa ni sawa na kuvuruga mchakato wa kupata
Katiba Mpya, kuiweka nchi rehani, na kufuja
fedha za walipakodi,
Katiba hiyo haikupita licha ya fedha lukuki za
watanzania kufujwa hadi sasa.
Madai ya sasa ya kumhoji Mbowe kuhusiana na
maandamano nchi nzima yalisababishwa na
msimamo wa kamati kuu ya chama hicho
unaowataka viongozi wa ngazi mbalimbali,
wafuasi na wapenzi wa chama hicho
kuandamana Septemba 1 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti
wa Chadema na kutangaza maazimio ya kamati
kuu Freeman Mbowe alisema kupitia kikao hicho
wamekubaliana kuanzisha operesheni ambayo
itafanyika kwa nchi nzima na kuwaagiza viongozi
wa wilaya zote nchini wa Chadema kuanza vikao
kujiandaa na operesheni hiyo.
“Tumefanya makubaliano ya pamoja na
kukubalina kuwa Septemba, 1 tutafanya mikutano
nchi nzima na mimi kama mwenyekiti nawaagiza
viongozi wa chama wa kila wilaya kuanza
kujiandaa na mikutano hiyo,
“Operesheni hii imepewa jina la UKUTA ikiwa na
maana ya Umoja wa Kupinga Udikteta nchini sio
ili kupinga mtu mmoja kuwa na sauti katika kila
jambo na kutaka kuliongoza yeye, hizi ni dalili za
udikteta,” alisema Mbowe.
Kamati kuu ya Chadema iliketi kwa dharura Julai
23-26 mwaka huu kwa ajili ya kujadili hali ya
siasa na uchumi wa taifa tangu serikali ya
awamu ya tano ilipoingia madarakani.
Kamati kuu ilitoa taarifa kuwa tangu utawala wa
awamu ya tano ulipoingia madarakani mwezi
Novemba, 2015 umechukua hatua mbalimbali za
kubinya Demokrasia na kuua dhana ya utawala
bora kwa njia mbalimbali.
Pia kamati kuu iliainisha makundi ya kijamii
ambayo tayari yameshaumizwa au kubinywa na
watanzania walio wengi wanakaa kimya kwa
sababu wao sio sehemu ya kundi husika ambalo
limenyimwa haki au kwa kuwa hajafikiwa moja
kwa moja.
Pamoja na mambo mengine, kamati kuu iliweka
wazi lengo la operesheni hiyo ni kuzuia matukio
ya ukandamizaji wa haki na demokrasia nchini,
kiliyodai kuwa yanafanywa na Rais Dk. John
Magufuli.
“Tangu kuanza kwa utawala wa awamu ya tano,
kuna matukio mbalimbali ya kubinya demokrasia
na kuua dhana ya utawala bora, na yapo makundi
ambayo tayari yameshaumizwa, huku Watanzania
wengi wakikaa kimya kwa sababu wao si sehemu
ya kundi lililominywa.
“Kwa kuwa wewe tayari umeshafikiwa, hauna
budi kujenga Ukuta ili kuzuia wengine
wasidhurike na utawala huu. Kwa kuwa wewe
hujafikiwa na ndiyo maana husemi wenzako
wanapofikiwa, basi njoo tujenge Ukuta ili
ukifikiwa awepo wa kusema,” alisema Mbowe.
Kutokana na hilo, aliwataka viongozi wa dini zote
pamoja na Watanzania wapenda amani,
kuungana na chama hicho kujenga Ukuta ili
kuzuia uchumi kuporomoka.
“Njoo tujenge Ukuta kuzuia udikteta huu, tujenge
Ukuta tuilinde Katiba yetu… Ukuta huu ni wa
wananchi wote bila kujali dini, kabila, chama cha
siasa au rangi,” alisema Mbowe.
Akizungumzia chimbuko la Ukuta, Mbowe alisema
umetokana na Rais Magufuli kupiga marufuku
safari zote za nje kwa watumishi wa umma,
kuamuru Mahakama Kuu iwahukumu
wafanyabiashara ambao wana kesi za kodi ili
Serikali ishinde.
Aidha Mbowe alisema sababu zilizowasukuma
kuanzisha Ukuta ni pamoja na mabalozi na
wanadiplomasia kuzuiliwa kukutana na viongozi
wa kisiasa bila kibali cha Serikali, watumishi wa
umma kufukuzwa ovyo bila utaratibu kwa
kisingizio cha kutumbua majipu bila kufuata
sheria na kanuni za utumishi wa umma na
mawakili kuunganishwa kwenye kesi za wateja
wao wanapokwenda kuwatetea.
Walimu kukatwa mishahara iwapo dawati
litavunjika kwenye shule yake, kupotezwa kwa
wana-CCM ambao watapinga kauli ya mwenyekiti
au kuwa na maoni tofauti, unyanyasaji na
udhalilishaji wa viongozi wa dini na wananchi wa
Zanzibar ni miongoni mwa sababu alizotaja
Mbowe.
“Historia inaonyesha duniani kote hakuna ambako
utawala uliwahi kuushinda ukuta wa wananchi,
na hii ndiyo nguvu ya umma, kila mmoja achukue
hatua popote alipo kujenga Ukuta,” alisema.
Kuhusu kufanyika kwa mikutano ya hadhara
Septemba Mosi, Mbowe amesema Kamati Kuu
imeagiza ngazi zote za chama kuanzia ya msingi,
kata, majimbo, wilaya, mikoa, kanda, mabaraza
na taifa kukaa na kufanya maandalizi ya
mikutano hiyo nchi nzima.
Haya yanajiri ikiwa ni siku kadhaa tangu Tundu
Lissu, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho
kutiwa mbaroni kwa madai ya uchochezi.chanzo mwanahalisi oneline.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top