Msanii Ali kiba ametoa msaada kwa ajili ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.soma zaid
Msanii wa muziki AliKiba amempiku Diamond
kwa kutoa tsh 21 Milioni kwa GSM Foundation
ikiwa ni siku chake toka muimbaji huyo wa
wimbo ‘Kidogo’ kutoa msaada wa tsh 20 Milioni
kwa ajili ya kusaidia jitihada za taasisi hiyo za
kutoa huduma ya upasuaji wa watoto wenye
vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo
‘Aje’, ameonyesha kuguswa na tatizo hilo ambalo
limekuwa likiwasababishia watoto ulemavu wa
kudumu.
“Nimeguswa sana na kampeni ya GSM
Foundationt katika kuwasaidia watoto wetu wa
Kitanzania wanaosumbuliwa na magonjwa ya
kichwa kikubwa na mgongo wazi. Toka
wameanza shughuli hii, mamia ya watoto
wameokolewa kutokana na taabu walizokuwa
wanazipata,” aliandika AliKiba kupitia instagram
yake.
Aliongeza, “Nimefurahi kutoa japo kidogo katika
niliichojaaliwa kuunga mkono kampeni
hizi.Nawasihi jamii yenye uwezo kila mmoja kwa
nafasi yake kutoa kidogo ili kuokoa maisha ya
watanzania.#SupportedByKiba #KingKiba,”
Kwa upande wa taasisi hiyo, wametoa ujumbe
wa shukrani kwa msanii huyo kwa kuguswa na
jitihada za taasisi hiyo za kusaidia watoto
aliokatika wakati mgumu.
“AliKiba tunashukuru sana, kwanza kwa
kututembelea katika ofisi yetu ya #
GSMFoundation na pili kwa mchango wako
uliotupatia wa kiasi cha shilingi milioni ishirini na
moja (21,000,000) ukiwa ni mchango wako na
kuunga mkono juhudi zetu za kuwafanyia
upasuaji watoto wanaosumbuliwa na magonjwa
ya kichwa kikubwa na mgongo wazi. Mwenyezi
Mungu akujalie kwa moyo wako na kukubariki
katika kila unalolifanya,” uliandika ukurasa wa
instagram wa taasisi hiyo.
0 comments :
Post a Comment