Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, August 11, 2016

Msanii Kajala atoa somo kwa wanawake au mabinti wanaolewa kwa tamaa ya fedha.soma zaid.

Msanii wa filamu nchini Kajala Masanja ambaye
kwa sasa yupo karibu sana na msanii Quick
Racka amefunguka na kusema kuwa alikurupuka
kukubaliana na mwanaume ambaye hakuweza
kumfahamu vizuri tabia zake baada ya yeye
kuhongwa gari aina ya Harrier.
Kajala alitoa ushuhuda huo kwenye kipindi cha
Friday Night Live ya (EATV) alipokuwa akiwapa
hamasa mabinti na wasichana kutokukurupuka
kwa kuangalia mali za wanaume bali wanapaswa
kujisomea ili baadaye waje kuwa na maisha yao
wenyewe, kwani yeye alikurupuka na kuolewa na
matokeo yake aliishia kufungwa gerezani kwa
sababu ya mwanaume wake.
“Ni kweli mfano mimi nilihongwa gari aina ya
Harrier nikajikuta nakubaliana na mwanaume
lakini baadaye nilikuja kujuta maana niliishia
gerezani, hivyo nawaomba mabinti wenzangu
tusikurupuke kwenye maamuzi, na wale
wasichana ambao wanasoma wanapaswa
kusoma ili baadaye waje kuwa na maisha ya
kwao wenyewe” alisema Kajala.chanzo EATV

0 comments :

Post a Comment

Back To Top