Mrema asema yeye ni mpinzi mtaarabu.soma zaid
Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino
Mrema amewaonya wapinzani wenzake kuacha
kupanga kufanya maandamano Septemba, 1 na
watumie muda wao kushirikiana na Rais
Magufuli kufanya kazi ili kuleta maendeleo kwa
watanzania.
Mrema ameyasema hayo wakati akizungumza
katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds
Fm na kusema kuwa wanatakiwa kufanya siasa
kama anayoifanya yeye ya kuwa mpinzani
mstaarabu ambaye anaunga mkono kazi
zinazofanywa na Rais Magufuli.
“Mimi ni mpinzani mstaarabu, upinzani wa
kijinga siutaki kama wewe ni mpinzani wa kweli
inatakiwa ukae bungeni ili kutoa matatizo ya
watanzania lakini sasa wao wanatoka ningekuwa
mimi nisingetoka, niwashauri tu wakae wafanye
kazi,” alisema Mrema.
Aidha Mrema aliwaonya Chadema kuacha
kupanga kufanya maandamano ya UKUTA kwani
rais wa sasa ana nia ya dhati kuwafanyia kazi
watanzania na kama wamekosa kazi ya kufanya
waende shambani kulima au kusaidia kutatua
tatizo la madawati.
“Rais ameshasema apewe muda kuleta
maendeleo kwa watanzania na yeye ndiyo
mwenye majeshi kama wamepanga kufanya
maandamano wasidhani kitawakuta kama
kilichonikuta mimi mwaka 1995, rais anataka tu
kazi kama hawana ya kufanya waende
mashambani kulima au wakatafute madawati,”
alisema Mrema.
0 comments :
Post a Comment