January 21, 2025
Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, September 3, 2016

Bodi ya mikopo kutoa fedha kwa waombaji chuo kikuu waliokidhi vigezo.soma zaid


Bodi ya Mikopo kumwaga fedha kwa
waombaji wote
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HESLB) imesema wale wote walioomba mkopo
mwaka huu na kukidhi vigezo watapewa.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq
Badru alisema hayo juzi mjini hapa wakati wa
hafla ya kukabidhi vyeti kwa watu watano
waliorejesha mkopo wa elimu ya juu kwa
mkupuo na kwa hiari.
Badru alisema idadi ya walioomba mkopo
mwaka huu ni wanafunzi 88,000 ambao bodi
itahakikisha wale wote waliokidhi vigezo,
wanapatiwa fedha kwa ajili ya elimu ya juu.
Mkurugenzi huyo ambaye amehimiza
walionufaika na mikopo kulipa madeni yao,
alisema mwaka jana, wanafunzi waliokopeshwa
ni 55,000.
Kuhusu waliopewa vyeti ikiwa ni hatua ya
kuwatambua, ni pamoja na mfanyakazi wa VETA
Shinyanga, Richard Jafu aliyerejesha kwa
mkupuo Sh 14,749,950 na Francis Mwilafi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo aliyelipa Sh
15,115,200.
Wengine ni Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga
aliyerejesha Sh 255,000; Profesa Peter Msoffe
ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha
Dodoma (UDOM) aliyerejesha Sh 1,430,749.
Mwingine ni Mbunge wa Biharamulo, Oscar
Mukasa ambaye kiasi alichorejesha hakikutajwa
ingawa mkurugenzi mtendaji wa HESLB, alisema
amerejesha kiasi kikubwa kwa mkupuo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao
walisisitiza umuhimu wa wanufaika wa mikopo
kuirejesha kwa hiari ili kuiwezesha bodi hiyo
kukopesha wanafunzi wengine.
Mbunge wa Biharamulo, Mukasa alishauri bodi
hiyo kuangalia uwezekano wa kurekebisha
vigezo kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi
watokao maeneo ya pembezoni kunufaika na
mikopo hiyo ya elimu. Kwa upande wake,
Mbunge wa Vwawa, Hasunga alisisitiza wabunge
wanaodaiwa warejeshe mkopo kwa mkupuo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top