Dhamira ya serikali kuhamia Dodoma ipo palepale ndani ya kipindi cha miaka 4.soma zaid
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
(mb) amesisitiza kuwa dhamira ya
Serikali kuhamia Dodoma ipo palepale
ndani ya kipindi cha miaka minne hatua
kwa hatua.
Akizungumza na waandishi wa habari
Septemba 2, 2016 wakati wa ziara yake
eneo la Makazi Mapya ya Mhe. Waziri
Mkuu Majaliwa Kassim yaliyopo Mlimwa
Dodoma, Waziri Mhagama alisema
“Watanzania wawe na amani, dhamira
yetu iko vizuri na kama Mhe. Rais
alivyosema na tunawahakikishia
kwamba ndani ya kipindi hicho sisi
tumeshajipanga kuhamamia mkoani
Dodoma hatua kwa hatua”.
Waziri Mhagama alieleza kuwa shughuli
za maendeleo hazitosimama kwa
kuzingatia mipango iliyopo na bajeti ya
Serikali, “Niwatoe wasiwasi kwamba
mipango yote ya maendeleo haitosimama
na shughuli zote za maendeleo
hazitozuiwa na ujio wa Serikali mkoani
Dodoma zitafanyika kama zilivyopangwa
na tutaendelea kuyafanya hayo kwa
kuzingatia Ilani ya uchaguzi ya mwaka
2015 Ibara ya 151 tumesema tunahamia
Dodoma na tutafanya hivyo”.Alisisitiza
Mhagama
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana
ameahidi kutekeleza usimamizi wa
maagizo ya Waziri ili kukamilisha ujenzi
wa barabara kwa wakati “kwa upande
wa mkoa kazi iliyobaki ni kuhakikisha
kuwa ujenzi wa barabara unakamilika
na tutakutana na Wakala wa Barabara
(TANROADS), Mamlaka ya Ustawishaji
Mji (CDA) na Manispaa ili kuona
shughuli hii tunaifanyeje kwa kutekeleza
maagizo hayo ikiwa ni sehemu ya
majukumu ya mkoa.”
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Jordan Rugimbana alimshukuru Waziri
Mhagama kwa kutembelea maeneo ya
makazi mapya ya Mhe. Waziri Mkuu na
Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma,”Namshukuru Mhe. Waziri
Mhagama, Manaibu Waziri na Ofisi yote
ya Waziri Mkuu kwa ziara hii na
kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi
wa Makazi Mapya ya Mhe. Waziri
Mkuu.”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb)
akifuatilia maelezo ya ramani ya Makazi
Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa
Kassim kutoka kwa Wataalam wa
maswala ya Ujenzi kulia kwake ni
Mhandisi Joseph Muhamba na wa
kwanza kushoto ni Bw. Keffa Chana
wakati wa Ziara yake katika makazi
hayo Septemba 2, 2016 Mlimwa Dodoma.
0 comments :
Post a Comment