Jarida la Forbose lasifu uwezo wa Ndege aina ya Bombardier.soma zaid
WAKATI Serikali ya Tanzania ikiwa
imenunua ndege mbili za aina ya
Bombardier Dash8 Q400 kutoka Canada,
imebainika na kusisitizwa kuwa ndege
hizo zina usalama mkubwa, zinatumia
mafuta kidogo na kutabiriwa kuwa nguzo
muhimu kwa usafiri wa bei chee wa ndani
ya nchi mbalimbali.
Hayo yamo katika makala iliyoandikwa na
kuchapishwa na jarida mashuhuri duniani
la Forbes ikiwa na anuani “Can
Bombardier’s Q400 Save Regional Air
Service in the US?” ambapo mwandishi
anafafanua faida za ndege hizo
ikilinganishwa na nyingine zinazofanya
usafiri wa ndani Marekani.
“Bombadia ina kasi nzuri na ya
kutosheleza mahitaji ya safari za ndani
kwa kiwango cha kuwa na faida zaidi
kibiashara ikilinganishwa na ndege
nyingine za aina yake kama ATR,”
linaandika Forbes.
Faida nyingine inayotajwa ya Bombardier
ni matumizi ya mafuta. Forbes
wanaandika kuwa ndege hizo zina uwezo
wa kutumia mafuta kidogo sana kiasi
kwamba hata bei ya tiketi zake itakuwa
chini na kuwasaidia abiria wengi wa
ndani.
“Kutumia kwake mafuta kiasi kunaifanya
Bombardier kuwa na ufanisi wa asilimia
kati ya 48 mpaka 50 za kuwa bora zaidi ya
ndege nyingine za ukanda huu,”
linaandika Forbes.
Forbes wanasisitiza kuwa kutokana na
gharama za matengenezo kupanda, na
gharama nyingine za uendeshaji ikiwemo
mishahara mizuri kwa marubani, kuna
uwezekano mkubwa kwa Bombardier
kuendeshwa kwa bei rahisi na ikauza
tiketi kwa bei rahisi zaidi kuliko ndege
nyingine.
“Kwa sasa tunakadiria kuwa ndege aina
ya Bombardia ndio zitakuwa mbadala na
zitashika njia nyingi za ndani (Marekani)
kwa kiasi cha asilimia 50 hadi 60 na
zitasaidia kurejesha usafiri uliositishwa
(kutokana na gharama kubwa kwa ndege
nyingine) katika viwanja takribani 20,”
linaandika zaidi Forbes.
Akikaririwa katika makala hiyo, Mike
Arcamone, Rais wa Masuala ya Biashara
wa Bombardier anasema wasiwasi wa
awali wa abiria kuhusu ndege hizo
kutumia mfumo wa turbo sasa umeondoka
kwa kuwa injini na dizaini ya kisasa ya
ndege hizo inaifanya isiwe na kelele kama
ilivyodhaniwa.
“Wanunuzi wengi wa ndege hizi
wamebaini kuwa hazina kelele na
watumiaji wengi wanaamini kuwa
zinaweza kuwa mbadala wa ndege
nyingine za bei nafuu,” anasema afisa
huyo kauli inayokubaliwa na wachambuzi
wa Forbes.
Tayari Serikali ya Tanzania imeahidi
kuleta ndege nyingine ya pili wiki hii
baada ya ile ya kwanza kuwasili nchini
wiki iliyopita ukiwa ni mkakati na
utekelezaji wa ahadi ya Rais John Pombe
Magufuli ya kulifufua Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL).
Kuwasili kwa ndege hizo kunaashiria
mengi lakini muhimu ni uthabiti wa ahadi
za Dkt. Magufuli akiwa ndani ya kipindi
cha mwaka mmoja wa uongozi wake,
ambapo mambo mengi makubwa ambayo
ameyaahidi ameanza kuyafanyiakazi na
kuwakuna wengi nchini na nje ya nchi.
0 comments :
Post a Comment