Neena yatangazwa kwa timu ya serengeti Boys.soma zaid
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Nape Moses Nnauye akizungumza na
waandishi wa Habari (hawapo Pichani) kuhusu
mchezo kati ya Serengeti Boys na Congo-
Brazaville utakaofanyika Septemba 18 katika
Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Nape Moses Nnauye ameahidi kutoa
shilingi laki tano kwa kila goli litakalofungwa na
timu ya Serengeti Boys katika mchezo wa
kuwania kufuzu fainali za Kombe la mataifa ya
Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17
utakaofanyika kesho katika Uwanja wa Taifa
dhidi ya Congo-Brazzaville.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar
es Salaam Mhe.Nape amesema milango ipo
wazi kwa wadau wengine wa michezo kujitolea
katika kuiwezesha timu na hivyo kufanya vizuri
katika mechi hii ambayo ni muhimu sana
kushinda ili kufuzu kwa fainali hizo.
“Hii timu ni yetu sote hivyo inahitajika tuimiliki,
tuepe nguvu, tuiombee ili iweze kufanya vizuri
na hatimaye kufuzu kuingia fainali kwa kuitoa
timu ya Congo-Brazzaville” alisema Mhe. Nape.
Aidha aliongeza kuwa kesho asubuhi atakutana
na wachezaji wa timu hiyo ili kuwapa maneno
ya faraja kabla ya kuanza kwa mechi na
kuwataka watanzania kujitokeza kwa wingi
uwanjani ili kuwapa motisha wachezaji kwa
kuwashangilia na kuwatia moyo.
Mbali na hayo Waziri Nape alitoa ufafanuzi
kuhusu matumizi ya kadi za kieletroniki
zilizozinduliwa hivi karibuni kwa kueleza kuwa
kadi hizo bado hazijaanza kutumika rasmi ili
zitaanza kutumiwa katika mchezo baina ya
Wabunge wa Simba na Yanga pamoja na Bongo
Fleva.
Timu ya Serengeti Boys inaundwa na vijana wa
Kitanzania wenye umri chini ya miaka 17
ambapo katika mchezo wa kesho watahitaji
ushindi na baadaye kufanya mechi ya
marudiano mnamo Oktoba 2 mwaka huu nchini
Congo-Brazzaville.
0 comments :
Post a Comment