Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ametangaa hali ya hatari baada ya mauaji ya watu 14.
Rais wa Filipino Rodrigo Duterte ametangaza
hali ya hatari baada ya mauaji ya watu 14
yaliyotokea kwenye mlipuko wa bomu katika mji
wa Davao nchini humo.
Abu Sayyaf anayejiita mwenye msimamo mkali
amedai kuhusika na shambulio hilo. Licha
Sayyaf kutangaza kuhusika, mamlaka za
usalama nchini humo zimeahidi kuangalia
watuhumiwa wengine zaidi.
Mlipuko huo ulitokea majira ya usiku karibu na
maeneo ya soko, chuo kikuu na hoteli yenye
hadhi ya nyota, na kuua watu 14.
Chuo hicho kinachofahamika kwa jina la Ateneo
de Davao University na hoteli Marco Polo,
inadaiwa kutumiwa na rais Duterte kwenye ziara
zake nyingi na hoteli hiyo ilitumika kwa ajili ya
mikutano wakati wa kampeni za Uchaguzi wake
wa kitaifa.
Rais Duterte aliviambia vyombo vya habari
nchini humo kuwa, amelazimika kutangaza hali
ya vurugu kutokana na vitendo vya kihalifu
vilivyotokea nchini humo.
Duterte leo amewaambia waandishi wa habari
katika mji wa Davao kuwa ‘Ni tishio dhidi ya
watu na dhidi ya taifa nitachukua hatua kali
dhidi ya waliohusika na shambulio hilo, nina
wajibu huu ili kulinda nchi hii .’
Msemaji wa Abu Sayyif alisema walihusika na
mlipuko huo, na kudai kuwa Kundi
linaloongozwa na Sayyif limetishia kuanzisha
mashambulizi baada ya wapiganaji wake 30
kuuawa katika mashambulizi ya kijeshi
yaliyotokea wiki iliyopita.
Hata hivyo, Duterte amesema wakaguzi
wanaendelea kuangalia watuhumiwa wengine
zaidi ili kuthibitisha kama wahalifu wa dawa za
kulevya walihusika.
“Hizi ni nyakati za ajabu, na mimi nina mamlaka
ya kuruhusu vikosi vya usalama wa nchi hii
kufanya upekuzi, na tutakabiliana na mgogoro
uliopo sasa,”
Aliongeza. “Kuna mgogoro katika nchi na
washirika wa madawa ya kulevya, ambao
wanafanya mauaji yasiyo halali na inaonekana
kuwa bado kuna mazingira ya vurugu kutoka
kwa wahalifu.”
Tangu uzinduzi wake kama rais wa kupambana
na wafanyabiashara wa dawa za kulevya
mwishoni mwa mwezi Juni,2016, watu 2,000
wameuawa hadi sasa.
0 comments :
Post a Comment