TANESCO wameanza kazi ya uboreshaji wa miundo mbinu wa umeme kwenye kituo kikubwa cha kupoaza umeme ubungo Dar.soma zaid
Wahandisi na mafundi wa Shirika la Umeme
Nchini Tanzania, (TANESCO), kwa kushirikia na
mafundi wa kampuni za Kijapani za Yachiyo
Engineering Co Limited, Takaoka na National
Construction Co. Limited, wameanza kazi y
uboreshaji miundombinu ya umeme kwenye kituo
kikubwa cha kupooza na kusambaza umeme cha
Ubungo jijini Dar es Salaam.
Kazi kubwa inayofanyika hivi sasa ni kubadilisha
laini kutoka umeme mdogo kwenda umeme
mkubwa, lakini pia kubadilisha vifaa vingine
muhimu ili kuwezesha usafirishaji umeme uweze
kuwafikia watumiaji katika ubora ulio juu.
“Ikumbukwe kwamba, hapa tulikuwa na laini
mbili (waya mbili) zilizokuwa na uwezo wa
kusafirisha umeme kiasi cha Megawati 120 kila
moja, kutoka hapa Ubungo kwenda kituo cha
Ilala, lakini kazi inayofanyika sasa, ni kubadili
njia hizo (waya za umeme), ambazo zitakuwa na
uwezo wa kupitisha kiasi cha umeme wenye
Megawati 220 kila moja,” alifafanua Meneja
Muandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika
hilo, ambaye pia ndiye Meneja wa wa Mradi wa
kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia
Theodory Bayona.
Kwa mantiki hiyo, kazi inayofanyika leo hii
itawezesha umeme utakaokuwa ukisafirishwa
kutoka hapa Ubungo kwenda Ilala, kuwa na
jumla ya Megawati 440 kwa laini zote mbili,
tofauti na hapo awali ambapo uwezo wa
kusafirisha umeme ulikuwa Megawati 240 tu,”
alisema.
Kazi ikikamilika wakazi wa jiji la Dar es Salaam,
watakuwa wakipata umeme wa uhakika, na ulio
bora, alifafanua Injinia Bayona.
Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la
Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), Leila
Muhaji, amewaomba wananchi kuwa wavumilivu
katika kipindi hiki ambapo Shirika linafanya
juhudi kubwa za kuwapatia umeme wa uhakika
wananchi kwa kuimarisha miundombinu yake.
“Ili kuwawezesha mafundi wetu kufanya kazi
katika mazingira salama, tutakuwa tukikata
umeme kuanzia leo hii Septemba, 3 na umeme
utakuwa ukikatika kuanzia saa 2 asubuhi na
kurejea saa 11 jioni kwa utaratibu na tarehe
kama ifuatavyo; Septemba 3-4, Septemba 10-11,
Septemba 17-18, na Septemba 24-25, 2016.”
Alifafanua Leila, na kuwaomba wananchi kuwa
wavumilivu katika kipindi hiki.
Mradi huu ulioanza Februari 2015 na
unaotarajiwa kukamilika Juni 2017
unatekelezwa na Serikali kupitia TANESCO kwa
ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA)
.
0 comments :
Post a Comment