Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, September 28, 2016

Waziri Profesa makame Mbarawa amewataka wadau wa sekta ya miundombinu kuchangamkia Fursa.soma zaid


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa
sekta ya miundombinu ya Reli na Barabara
kushirikiana na Serikali katika kuchangamkia
fursa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
sekta hiyo hapa nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Saba wa
wadau wa Sekta hiyo, Prof. Mbarawa amesema
kwa sasa Serikali kupitia Rais wa Awamu ya
Tano inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo
ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Tanga hadi
nchini Uganda, ujenzi wa barabara ya kulipia wa
Dar es Salaam-Chalinze KM 144 (Dar-Chalinze
Express way) na ujenzi wa reli ya kati hivyo ni
muhimu kwa wadau hao kutumia mkutano huo
katika kuijadili miradi hiyo.
“Ni matumaini yangu katika mkutano huu
mtajadili kwa pamoja namna ya kushirikiana na
Serikali katika kutekeleza fursa za ujenzi wa
miundombinu hapa nchini ikiwemo kuungana na
Serikali (Public Private Partnership) au kwa njia
nyingine yoyote”, amesema Waziri Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Aidha, Profesa Mbarawa amewataka wadau hao
kutumia mkutano huo wa siku mbili kujadili
namna bora ya kutunza na kuboresha
miundombinu ya reli na barabara ili kuweza
kudumu kwa muda mrefu.
Amesisitiza wadau hao kuja kwa wingi nchini na
kuwekeza katika sekta hiyo ili kupanua
ushindani wa kibiashara katika soko la kitaifa na
kimataifa.
Wazri Mbarawa amebainisha kuwa Serikali
inaendelea kutafuta pesa kutoka kwa wadau
mbalimbali na kushirikisha taasisi binafsi
kupitia mpango wa kushirikiana baina ya Serikali
na Taasisi hizo (Public Private Partnership ) ili
kutekeleza miradi ya miundombinu ya reli na
barabara nchini.
Mwenyekiti wa wadau wa barabara Tanzania Eng.
Abdul Awadhi akiongea na wadau wa miundombinu
ya barabara na reli wakati wa mkutano wa Saba wa
wadau hao, uliofanyika jijini Dar es salaam.
Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa
Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia
(TAZARA) Eng. Bruno Ching’andu amesema
kuwa licha ya TAZARA kuwa na treni za umma
zinazotoa huduma za usafiri nchini bado
inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo
uhaba wa fedha katika uendeshaji wa shirika
hilo ikiwemo gharama za ujenzi na ukararabati
wa mabehewa.
Mkutano huo wa siku mbili umewakutanisha
wadau wa miundombinu ya barabara na Reli
kutoka Taasisi za Serikali na wadau mbalimbali
wa sekta hiyo kutoka ndani na nje ya nchi lengo
likiwa ni kujadili kwa pamoja namna ya
kuboresha miundombinu hiyo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top