Idara ya Uhamiaji kuajiri askari na msofisa 297 .soma zai
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia
Idara ya Uhamiaji imekamilisha taratibu za
kuwapatia ajira askari na maofisa 297
waliohitimu mafunzo yao ya awali ya Uhamiaji
Juni mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa
wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira
ilifafanua kuwa askari na maofisa 181 walianza
kupata mishahara yao Oktoba mwaka huu na
waliobaki 116 watapata mishahara yao mwezi
huu baada ya taratibu zote za ajira zao
kukamilika.
Alisema wameshaingiza taarifa zao za
kiutumishi ambazo ni vyeti vya taaluma, vyeti
vya kuzaliwa, barua za ajira na fomu za
kudhibiti ajira kwenye mfumo shirikishi wa
taarifa za kiutumishi na mishahara ambalo ni
hitaji la kisheria.
“Kukamilika kwa taratibu hizo kutawezesha
watumishi wengine ambao hawakupata
mshahara mwezi uliopita kupata mshahara wao
mwezi huu na hivyo kufanya watumishi wote
kupata mishahara yao,” ilisema taarifa hiyo ya
Rwegasira.
Alisema kukamilika kwa taratibu za ajira kwa
askari na maofisa 181 walioanza kulipwa
mishahara yao ya Oktoba kulienda sambamba
na kupatiwa barua zao za ajira.
Alifafanua kuwa taratibu za ajira kwa askari na
maofisa hao 297 zilianza kufanyika Agosti
mwaka huu baada ya vyombo vya ulinzi na
usalama vilivyoko ndani ya wizara hiyo kupata
idhini ya kuendelea na mchakato wa ajira kwa
askari na maofisa waliokuwa wamehitimu
mafunzo ya awali ya kijeshi kwenye vyuo
mbalimbali vya majeshi chini ya wizara hiyo.
Alisema baada ya kupata idhini ya kuendelea na
mchakato wa ajira, askari na maofisa hao 297
wote walipangiwa vituo vya kazi katika mikoa
mbalimbali nje ya mkoa wa Dar es Salaam
kulingana na mahitaji ya kila mkoa.
0 comments :
Post a Comment