Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, January 10, 2017

Hutuba ya Barrack Obama yawaliza wamarekani wengi.soma zaid

Barrack Obama aliangazia demokrasia
Marekani katika hotuba yake ya mwisho
Rais wa Marekani Barack Obama
amewahimiza Wamarekani kuitetea
demokrasia, kwenye hotuba yake ya
mwisho kama rais wa Marekani mjini
Chicago.
"Kwa kila kipimo, Marekani sasa ni bora
zaidi, na ina nguvu zaidi" kuliko
ilivyokuwa miaka minane iliyopita
alipochukua madaraka, amewaambia
maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika
mjini humo.
Hata hivyo, "demokrasia inatishiwa kila
inapokosa kutiliwa maanani".
Amewaomba Wamarekani wa kila asili
kuangazia mambo kutoka kwa msimamo
wa wengine, na kusema kwamba "lazima
tuwategee sikio wengine na kusikia".
Rais Obama ndiye rais wa kwanza nchini
Marekani wa asili ya Afrika na
alichaguliwa mwaka 2008 akiahidi
kurejesha matumaini na kutekeleza
mabadiliko.
Mrithi wake Donald Trump ameahidi
kubatilisha baadhi ya sera kuu
alizofanikisha Bw Obama, 55.
Bw Trump ataapishwa tarehe 20 Januari.
Umati ulisema kwa sauti "miaka minne
zaidi" lakini kiongozi huyo alizipuuzilia
mbali.
"Siwezi kufanya hivyo," alisema.
"Marais wa Marekani wanaruhusiwa
kuongoza kwa mihula miwili pekee katika
katiba."
Bw Obama, aliyeonekana mchangamfu,
alisema utamaduni wa kukabidhi
madaraka kwa warithi kwa njia ya amani
ni moja ya mambo makuu
yanayotambuliwa katika demokrasia
Marekani.
Lakini amesema kuna mambo matatu
yanayotishia demokrasia Marekani -
ukosefu wa usawa kiuchumi, mgawanyiko
kwa misingi ya rangi na hatua ya baadhi
ya makundi kwenye jamii kujitenga na
kuwa na misimamo ambayo haiongozwi
na ukweli.
Akikamilisha hotuba yake, amesema ombi
lake moja la mwisho kabisa kwa
Wamarekani akiwa kama rais ni:
"Nawaomba muwe na imani. Si katika
uwezo wangu wa kuleta mabadiliko - bali
katika uwezo wenu."

0 comments :

Post a Comment

Back To Top