Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, January 24, 2017

Kauli ya Uhuru Kinyatta imetoa mwanga kwa wapinzani.soma zaid

Alisema hayo alipokuwa anazungumza na
waandishi wa habari katika Ikulu Ndogo ya
Sagana, akiwa kwenye ziara maeneo ya
Murang’a, Nyeri, Laikipia, Meru na Isiolo kuhimiza
wananchi wajiandikishe kwenye kitabu cha
kupigia kura
Nairobi. Rais Uhuru Kenyatta amesema kwamba
atakabidhi madaraka kwa amani ikiwa
atashindwa na mgombea urais wa upinzani
kwenye Uchaguzi Mkuu ujao utakaofanyika Agosti
8 mwaka huu.
Alisema hayo alipokuwa anazungumza na
waandishi wa habari katika Ikulu Ndogo ya
Sagana, akiwa kwenye ziara maeneo ya
Murang’a, Nyeri, Laikipia, Meru na Isiolo kuhimiza
wananchi wajiandikishe kwenye kitabu cha
kupigia kura
“Nitakubali lolote litakaloamuliwa na wananchi
kwani enzi za marais kung’ang’ania madaraka
zimeshapita,’’ alisema.
Aliongeza, “Enzi hizo zilipita. Enzi hizo haziko
tena kwa sababu katiba inasema Rais anatakiwa
kutawala kwa vipindi viwili vya miaka mitano kila
kimoja,” alisema.
Kuiba kura
Rais Kenyatta alisema kauli za viongozi wa
upinzani wanaosema kwamba Jubilee inapanga
kuiba kura kwa sababu haitaki kuondoka
madarakani siyo za kweli.
‘’Baadhi yao wanadai huenda Jubilee ikabadilisha
katiba ili kuirudisha Kenya katika enzi za chama
kimoja cha kisiasa, hasa baada ya vyama tanzu
vya muungano wa Jubilee kuvunjwa kuunda
Jubilee Party’,’ alisema.
Rais Kenyatta aliwahimiza vijana wajisajili kwa
wingi kuwa wapigakura ili waweze kushiriki
Uchaguzi Mkuu ujao.
Rais aliitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka
(IEBC) izishinde kwenye vituo bali wazunguke
kuwaandikisha watu wanaoishi kwenye maeneo
ya wafugaji.
Mudavadi
Akiwa Busia, kiongozi wa chama cha Amani
National Congress (ANC), Musalia Mudavadi
alitoa changamoto kwa Rais Kenyatta aagize
idara ya kusajili watu itoe vitambulisho katika
muda wa siku tatu.
Alisema agizo hilo linatakiwa kutekelezwa kote
nchini wala si katika ngome za Jubilee pekee ili
kuwe na usawa kwenye Uchaguzi Mkuu wa
Agosti 8.
Akiwa Baringo, Naibu Rais William Ruto alisema
chama cha Jubilee kitashinda urais kwa sababu
ya rekodi yake ya maendeleo, aliwataka wafuasi
wa chama hicho wasiwe na wasiwasi.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top