Morogoro hapatoshi polisi watumia mabomu kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA.soma zaid
Jeshi la polisi mkoani Morogoro
limelazimika kutumia mabomu ya machozi
na mbwa kuwatawanya wananchi wa kata
ya Kiwanja cha ndege waliofika katika
kituo cha kutangazia matokeo ya
uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata
hiyo.
Hali hiyo imeibuka mara baada ya
mgombea wa udiwani kwa tiketi ya
CHADEMA Salum Milindi kufika katika
kata hiyo akiwa amenyanyua mikono juu
na kutaka kuingia ndani ya chumba cha
matokeo kwa mujibu wa sheria huku
akizuiliwa na jeshi la polisi.
Mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM
Isiaka Sengo aliibuka kidedea kwa kupita
mpinzani wake wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo CHADEMA Salum Milindi
kwa kura 192 ambapo msimamizi
msaidizi wa uchaguzi Shabani Duru
amemtangaza Isiaka Sengo kuwa diwani
wa kata hiyo.
Awali wakizungumza na ITV wasimamizi
katika vituo wameeleza changamoto zilizo
kuwepo ikiwa nipamoja na wananchi
kutojitokeza kwa wingi.chanzo itv
0 comments :
Post a Comment