Walimu wakuu 21 wilayani Ukerewe mkoani Mwanza Wamevuliwa madaraka kisa.soma zaid
Walimu wakuu 21 wa shule za msingi
katika halmashauri ya wilaya ya Ukerewe
mkoani Mwanza wamevuliwa madaraka
kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo
kuisababishia serikali hasara ya mamilioni
ya fedha kwa kuruhusu usajili wa
wanafunzi hewa pamoja na matumizi
mabaya ya madaraka.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya
wilaya ya Ukerewe,Frank Bahati amesema
amelazimika kuchukua uamuzi huo baada
ya walimu hao kushindwa kuwajibika
ipasavyo na kukosa umakini katika
usimamizi wa maendeleo ya
shule,ikiwemo taaluma na miradi ya shule
pamoja na vitendo vya ukiukwaji wa
maadili.
Amedai kuwa uzembe wa walimu wakuu
hao,pia umesababisha shule tano za
msingi wilayani humo kufungwa kwa
kukosa vyoo,baada ya walimu hao
kushindwa kutekeleza agizo lake la
kuwasilisha mpango mkakati wa kutatua
baadhi ya changamoto katika shule zao
ikiwemo ujenzi wa vyoo na vyumba vya
madarasa.
Halmashauri ya wilaya ya ukerewe
inayoundwa na jumla ya visiwa 38 ina
shule za msingi za serikali 123,walimu
1600 na wanafunzi 102,114.
Chanzo: ITV
0 comments :
Post a Comment