January 18, 2025
Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, February 1, 2017

Hii ni nini tena Bombadier Q dash400 soma zaid

Zaidi ya abiria 70 wa ndege ya Bombadier Q
dash 400,waliokuwa wakisafiri kutoka jijini
Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam jana majira
ya saa moja usiku,wameshindwa kusafiri kwa
kutumia ndege hiyo kutokana na kupata hitilafu
kwenye moja ya injini zake.
Kaimu Meneja wa uwanja wa ndege Mwanza
David Matovolwa amesema kutokana na ndege
hiyo yenye namba za usajili 5H TCB, kupata
hitilafu ikiwa inataka kunyanyuka kwenye
barabara ya kutulia na kurukia ndege ( runway ),
ilibidi abiria kubadilishiwa ndege iliyotoka Dar es
salaam ambapo waliweza kuondoka majira ya saa
saba kasorobo usiku huo huo.
Akithibitisha ndege hiyo kupata hitilafu,
Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la ndege Tanzania
( ATCL ), Mhandisi Emmanuel Koroso ameiambia
ITV kwa njia ya simu kwamba ndege hiyo
imeondoka uwanja hapo hii leo majira ya saa
4.30 asubuhi kuelekea jijini Dar es salaam ikiwa
haina abiria baada ya mafundi kuifanyia
matengenezo ya awali.
Shirika la ndege Tanzania lilizindua rasmi safari
za ndege zake aina ya Bombadier Q dashi 400
kati ya Dar es Salaam na Mwanza Oktoba mwaka
jana, ambapo ndege hiyo iliwasili mwanza kwa
mara ya kwanza saa 10.45 jioni ikiwa Katibu
mkuu wa Wizara ya ujenzi,uchukuzi na
mawasiliano Leonard Chamriho na kupokelewa na
mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.chanzo redio one.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top