Breaking News
Loading...

Advert

Monday, February 20, 2017

Zitto ziarani nchini Kenya kukagua miradi ya( IMF)soma zaid


Zitto Ziarani Nchini Kenya
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto yupo nchini Kenya kwa
ziara ya ukaguzi wa miradi ya Benki ya Dunia na
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Ziara hii ni
sehemu ya kazi za Mtandao wa Wabunge wa
Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia
(WB). Katika ziara hii kuna jumla ya wabunge 25
kutoka nchi mbalimbali duniani. Tanzania
inawakilishwa na Mbunge wa Kigoma Mjini na
Mbunge wa Sikonge ndugu Joseph Kakunda.
Katika ziara hiyo wabunge wanakagua miradi
mbali mbali inayotekelezwa na mashirika hayo na
namna gani miradi hiyo inachochea maendeleo
ya nchi husika. Benki ya Dunia Ina miradi ya
thamani ya USD 2.3 bilioni (sawa na wastani wa
Shilingi Trilioni 5) nchini Kenya. Wabunge
watakutana na Asasi za kiraia na sekta binafsi ya
Kenya. Upande wa Serikali watakutana na Waziri
wa Fedha, Gavana wa Benki Kuu na tume ya
mipango.
Asubuhi ya Leo ndugu Zitto alimtembelea
bungeni Spika wa Bunge la Kenya, Mheshimiwa
Justin Bedan Njoka Muturi. Pichani akiwa pamoja
na Spika Muturi (katikati) pamoja na Mbunge wa
Bunge la Uganda, mheshimiwa Nandala Nandala -
Mafabi (kulia) ambaye pia ni Katibu Mkuu wa
Chama cha Forum for Democratic Change (FDC)
cha Uganda kinachoongozwa na ndugu Kizza
Besigye. Mafabi naye ni mjumbe wa Mtandao wa
Wabunge wa IMF na Benki ya Dunia (WB).
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu
Zitto, ni mwanachama mwandamizi wa Mtandao
wa Wabunge wa IMF na Benki ya Dunia (WB)
kwa muda wa miaka 8 Sasa.
Imetolewa na Ofisi ya Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
Februari 20, 2017

0 comments :

Post a Comment

Back To Top