Rais Trump aapa kufufua ari na bidii ya wamarekani.soma zaid
Rais Donald Trump amehutubia wabunge wa
Marekani muda mfupi uliopita ambapo ameahidi
kufufua nguvu na bidii ya Wamarekani.
Amesema kwa muda mrefu, Wamarekani wa
kipato cha kati wamekuwa wakipungua na
miundo mbinu imedorora, huku maovu kama vile
uhalifu na ulanguzi wa dawa za kulevya kupitia
mipaka ya Marekani yakiendelea kushamiri.
Bwana Trump amesema ataliomba bunge
kuidhinisha bajeti ya dola trilioni moja kwa lengo
la kuwekeza katika miundo mbinu ya taifa hilo.
Ameahidi kupunguza kodi inayotozwa kampuni za
Marekani, na pia kupunguza kodi kwa
Wamarekani wa kipato cha kati.
Aidha rais Trump amesema kwamba atabadilisha
mfumo wa uhamiaji ulioko sasa ambapo watu
walio na ujuzi wa chini wanaruhusiwa kuingia
Marekani, na kusema kwamba wahamiaji
wanaoonekana kwamba wana ujuzi wa hali ya juu
na wanastahili kuingia Marekani, wataruhusiwa.
Anasema kazi yake si kulinda ulimwengu, bali ni
kulinda Marekani.
Amesema ataunga mkono muungano wa mataifa
yanayojihami ya NATO.
Amesisitiza kwamba Marekani itafanya kazi na
washirika wake kuangamiza kundi la kigaidi la
Islamic state.
Wakati wabunge wa Republican wakishangilia na
kufurahia hotuba hiyo, wabunge wa democrat
waliketi kimya bungeni, na baada ya hotuba
kukamilika, mmoja wao akasema hotuba ya
Trump haikuwa ya kuunganisha.
0 comments :
Post a Comment