Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, March 1, 2017

Uchungu w Njaa:Upungufu wa chakula Tanzani.Ripot ya Twaweza.soma zaid


Wiki na miezi iliyopita kumekuwepo na
mijadala mizito ya kisiasa na kitaifa juu ya
masuala ya upungufu wa chakula
Tanzania. Taaarifa za upungufu wa
chakula mwanzoni zilikataliwa na viongozi
wa juu wa serikali lakini baadae walikiri
kuwepo kwa upungufu wa chakula nchini.
Mwishoni mwa mwezi Januari 2017,
Waziri wa Chakula, Mifugo na Uvuvi, Dk.
Charles Tizeba aliliambia bunge kwamba
utafiti uliofanywa na Wizara kwa
kushirikiana na wadau kadhaa 1 ,
umegundua kwamba Wilaya 55 (kati 169
za Tanzania Bara na Visiwani) zilikumbwa
na njaa, na tani “35,491 za nafaka
zinahitajika kusambazwa kati ya mwezi wa
pili na wa nne mwaka 2017 ili kukabiliana
na upungufu huo uliowakumba watu
1,186,028” 2 katika Wilaya hizo.
Waziri Tizeba alilalamikia kupanda kwa
bei za vyakula katika maeneo mengi na
alisema hii inasababishwa na
wafanyabiashara wasio waaminifu
wanaotumia mianya ya njaa, pamoja na
uhitaji mkubwa wa mahindi katika nchi
jirani. Matokeo yake ni kusababisha bei
za ndani kupanda. Aliongeza kwamba
“Serikali imeanza kuchukua hatua
kudhibiti hali hiyo ambayo ni pamoja na
kutoa chakula kutoka hifadhi za taifa na
kuuza kwa bei nafuu katika maeneo yaliyo
athirika.”
Sintofahamu hii juu ya hali ya chakula
nchini imetokea katika kipindi ambacho
uchumi wa Tanzania umekua kwa kasi
nzuri ya asilima saba kwa mwaka. Lakini
ukuaji huu haujafanikiwa kuondoa
umasikini kwa kiwango kilichotarajiwa na
wengi. Asilimia 68 ya wananchi bado
wanaishi chini ya kiwango cha umasikini
cha $1.25 kwa siku 3 . Pamoja na hayo
kiwango cha udumavu kimeendelea
kuonekana kwa watoto chini ya miaka 5
4 , ukiachilia mbali mafanikio madogo
yaliyopatikana katika miaka ya karibuni
kwenye utoaji wa lishe nchini. Ofisi ya
Taifa ya Takwimu ya Tanzania (NBS) na
UNICEF wanakadiria kuwa robo tatu ya
watoto wote wa Tanzania asilimia 74)
wanaishi kwenye umasikini mkubwa 5 .
Muhtasari huu unawasilisha takwimu za
maoni ya wananchi na uzoefu wao katika
hali ya upungufu wa chakula na sababu
zake. Ni kaya ngapi na jamii zipi ambazo
zimekumbwa na njaa? Ni vyakula vipi
vilivyo adimu kupatikana? Na ni kwa
namna gani bei za vyakula zimepanda
ikilinganishwa na miezi michache
iliyopita?
Takwimu za muhtasari huu zimetokana na
utafiti wa Twaweza wa Sauti za Wananchi.
Sauti za Wananchi ni utafiti wenye
uwakilishi mkubwa unaotumia simu za
mkononi. Uwakilishi huu ni wa Tanzania
bara. Maelezo zaidi juu ya utafiti huu
yanapatikana katika tovuti ya
www.twaweza.or.tz/sauti . Takwimu za
muhtasari huu zilikusanywa katika awamu
ya pili ya kundi la pili la Sauti za
Wananchi.
1. Wahojiwa 1,800, awamu ya 13 ya
kupigiwa simu kwa kundi hili la
wahojiwa, kati ya tarehe 14 - 26
Septemba 2016.
2. Wahojiwa 1,610, awamu ya 16 ya
kupigiwa simu kwa kundi hili la
wahojiwa, kati ya tarehe 9 - 15
Februari 2017.
Matokeo makuu ni:
Kaya nane kati ya kumi (asilimia 80)
zimeripoti kwamba kipato chao
hakikidhi mahitaji yao ya kila siku.
Kaya nane kati ya kumi (asilimia 79)
huweka akiba ya chakula kwa ajili ya
kijitosheleza ifikapo vipindi vya njaa.
Wahojiwa wengi wa Sauti za Wananchi
(asilimia 78) wanaripoti upungufu wa
chakula katika maeneno wanayoishi
Bei ya mahindi imepanda mara mbili
katika kipindi cha miaka miwili na
kusababisha ongezeko la bei katika
bidhaa.
Kaya saba kati ya kumi (asilimia 69)
zilihofia kukumbwa na njaa katika
kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Hali ya upungufu wa chakula imekua
mbaya zaidi katika kipindi cha mwezi wa
Septemba mwaka 2016 hadi Februari,
2017.
Mambo nane muhimu kuhusu hali ya
chakula Tanzania
Jambo la 1: Kaya nane kati ya kumi
zimeripoti kwamba kipato chao hakikidhi
mahitaji yao ya kila siku.
Mwezi Septemba mwaka 2016 kaya nane
kati ya kumi (asilimia 80) ziliripoti kuwa
na kipato kisichokidhi mahitaji yao ya kila
siku. Takwimu hizi zinatofautiana kidogo
katika kaya za mijini na zile za vijijini au
kati ya kaya masikini na kaya tajiri.
Kielelezo cha 1: Je kipato
kinachopatikana katika kaya kinatosha
kukidhi mahitaji ya kila siku ya nyumbani?
Chanzo cha takwimu: Utafiti wa Sauti za
Wananchi - Awamu ya 13 (Septemba
2016)
Kaya tano kati ya sita (asilimia 85)
zinasema kwamba kipato kinapopungua
wanalazimika kubana matumizi. Idadi
ndogo inasema watakopa bidhaa (asilimia
6) na wengine huripoti kwamba watakopa
fedha zaidi (asilimia 2).
Walipoulizwa kukadiria ni kiasi gani cha
fedha kingetosha kwa ajili ya mahitaji ya
kaya ya kila siku, wastani wa makadirio
yote yalikua shilingi 1,777 kwa
mwanakaya au shilingi 10,662 kwa kila
kaya 6 . Kwa mwanakaya anaeishi mjini
makadirio yalikuwa juu kidogo (shilingi
2,247) kuliko kijijini (shilingi 1,579).
Makadirio pia yalikuwa makubwa zaidi
kutoka kwenye kaya zenye uwezo
(asilimia 20 ya waliokuwa na utajiri wa
juu sana - Shilingi 2,304) ukilinganisha na
kaya masikini (asilimia 20 ya waliokuwa
na umasikini wa chini kabisa - Shilingi
1,577).
Jambo la 2: Wananchi tisa kati ya kumi
wanaona ni jukumu lao wenyewe
kuhakikisha wana fedha za kutosha za
kukidhi mahitaji ya kaya zao
Idadi kubwa ya wananchi (asilimia 87)
wanasema iwapo watakosa fedha za
kukidhi mahitaji ya chakula kwa ajili ya
familia zao, hawatarajii watu wengine
kulichukua jukumu hilo. Hata hivyo,
asilimia 17 ya wanawake na asilimia 9 ya
wanaume wangetarajia msaada kutoka
nje.
Kielelezo 2: Iwapo ungekuwa huna pesa
za kukidhi mahitaji ya chakula kwa ajili ya
familia yako pamoja na kaya yako, je
unadhani ni jukumu la mtu kukusaidia au
ni jukumu lako mwenyewe?
Chanzo cha takwimu: Utafiti wa Sauti za
Wananchi - Awamu ya 13 (Septemba
2016)
Miongoni mwa wale wananchi wachache
(asilima 13) wanaofikiri kwamba ni
jukumu la mtu mwingine kuwasaidia
katika hali hiyo, nusu yao (asilimia 49)
wamesema ni wajibu wa serikali kutoa
msaada. Idadi ndogo wamesema ni wajibu
wa wanandugu (asilimia 36) au marafiki
na majirani (asilimia 7).
Jambo la 3: Katika kipindi cha mwaka
mmoja uliopita kaya moja kati ya nne
imepokea fao, faida au pesa kutoka
kwenye miradi ya serikali
Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita
kuanzia mwezi wa tisa 2015 mpaka mwezi
wa tisa 2016, asilimia 25 ya kaya
zimepokea fao, faida au pesa kutoka
katika vyanzo vifuatavyo:
Sare za shule, kadi ya matibabu, chakula
na kadhalika kutoka kwenye Mpango wa
Watoto Wanaoishi kwenye Mazingira
Magumu
Nafaka za bure kutoka kwa viongozi wa
kijiji na Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi Ya
Chakula (NFRA)
Chakula cha shule kinachotolewa na
Mpango wa Chakula Shuleni
Kazi za jamii zinazotolewa na Tanzania
Social Action Fund (TASAF)
Pesa zinazotolewa na TASAF kwa ajili ya
kunusuru kaya masikini
Vocha za mbolea/mbegu zinazotolewa
na Mpango wa Taifa wa Ruzuku na
Kilimo
Malipo ya mafao kutoka Mfuko wa
Pensheni wa Taifa (NSSF)
Malipo ya mafao kutoka Mfuko wa
Pensheni wa Watumishi wa Umma
(PSPF)
Kielelezo 3: Mafao au faida
zilizopokelewa ndani ya kipindi cha miezi
12 iliyopita
(Asilimia ya kaya zinazopokea mafao
haya)
Chanzo cha takwimu: Utafiti wa Sauti za
Wananchi - Awamu ya 13 (Septemba
2016)
Jambo la 4: Kaya nane kati ya kumi
huweka akiba ya chakula
Kaya nane kati ya kumi (asilimia 79)
zimeripoti kwamba wana hifadhi chakula
kwa ajili ya dharura au kuepukana na
njaa. Wananchi wengi zaidi wa vijijini
huhifadhi (asilimia 87) kuliko wa mijini
(asilimia 61) na kaya masikini huhifadhi
kuliko kaya tajiri. Uhifadhi wa chakula pia
uko juu kwa kaya ambazo hutegemea
zaidi kilimo kama sehemu kubwa ya
kipato chao (asilimia 92) kuliko kaya
ambazo hutegemea vyanzo vingine vya
mapato kama vile biashara au ajira
(asilimia 49).
Kielelezo cha 4: Je, kaya yako huhifadhi
chakula kwa ajili ya matumizi wakati wa
dharura au njaa?
(Asilimia iliyojibu ndiyo)
Chanzo cha takwimu: Utafiti wa Sauti za
Wananchi - Awamu ya 16 (Februari 2017)

0 comments :

Post a Comment

Back To Top