Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, March 2, 2017

Wanafunzi 11 wajeruhiwa baada ya jengo wanalosomea kuezuliwa na mvua.soma zaid

Wanafunzi kumi na moja wanaosoma shule ya KASISI ëAí iliyopo kata ya ILOLANGULU wilayani UYUI mkoani TABORA wamejeruhiwa baada jengo wanalosomea lenye vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja wa walimu kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha katika baadhi ya maeneo ya kata hiyo. Akizungumza na channel ten diwani wa kata ya ILOLANGULU MOHAMED LINSO amesema wanafunzi wawili kati ya kumi na moja waliojeruhiwa walilazimika kupelekwa hospitali ili kupatiwa matibabu zaidi. Kutokana na changamoto hii wanafunzi sasa wanalazimika kutumia vyumba viwili tu vya madarasa hali ambayo itaathiri maendeleo yao ya elimu. Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya UYUI SAIDI NTAHONDI amewataka wananchi wa kata ya ilolangulu kushikiana ili waweze kurejesha jengo katika hali yake na asiwepo atakayekwamisha zoezi hilo

0 comments :

Post a Comment

Back To Top