Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, April 20, 2017

Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamta msanii Agnes Masogange.soma zaid

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
imetoa hati ya kumkamata msanii, Agnes
Gerald maarufu kama Masogange kwa
kushindwa kuhudhuria kwenye kesi ya
kutumia dawa za kulevya inayomkabili.
Hati hiyo ilitolewa jana mbele ya Hakimu
Mkazi mkuu, Wilbroad Mashauri, wakati
kesi hiyo ilipotajwa.
Wakili wa Serikali, Adolf Mkini alidai
mahakamani hapo kwamba upelelezi wa
kesi hiyo upo hatua za mwisho, lakini
mshtakiwa, wadhamini wake na wakili
wake hawakufika hivyo wakili Nkini
akaomba mahakama itoe hati ya
kumkamata mshtakiwa huyo kwa sababu
ni mara ya pili ameshindwa kufika
mahakamani hapo.
Hakimu Mashauri alikubali maombi ya
wakili wa Serikali na kutoa hati ya
kumkamata mshtakiwa ambaye ni
Masogange.
Msanii huyo aliwahi kuonywa akitakiwa
aheshimu mahakama kutokana na
kutokuwapo kwenye kesi yake ilipotajwa.
Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka
2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya
Februari 7 na 14 mwaka huu, katika
maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar
es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina
ya heroin(Diacety Imophine). Pia inadaiwa
kati ya Februari 7 na 14, 2017 alitumia
dawa za kulevya aina ya oxazepam.
Chanzo: Mtanzania

0 comments :

Post a Comment

Back To Top