Mali za Said Lugumi za kamatwa kwa kudaiwa kodi na TRA. Soma zaid
Kampuni ya Yono Kupitia TRA
yamekamata majumba matatu ya Lugumi
yaliyoko Ndege Beach Mbweni kwa
kudaiwa kodi ya zaidi ya Bilioni 14.
Nawasilisha kutoka MINJINGU.
=======
Kampuni ya udalali ya Yono, imefanikiwa
kukamata mali za wafanyabiashara
wanaodaiwa kodi ya serikali inayofikia
zaidi ya Sh bilioni 68.1. Operesheni ya
kukamata mali hizo kwenye maeneo
mbalimbali ndani na nje ya Jiji la Dar es
Salaam imefanywa ndani ya wiki moja.
Katika operesheni hizo maofisa wa Yono
wamekuwa wakishirikiana na maofisa wa
Mamlaka ya Mapato(TRA), ambayo ndiyo
imeipa kampuni hiyo kazi ya kukusanya
kodi kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Yono, Scholastica Kevela,
Yono imepewa kazi na TRA kukusanya
madeni yake ya kodi kwenye mikoa ya Dar
es Salaam, Pwani Njombe, Mbeya, Iringa
na Zanzibar.
Aliwataka watanzania kuunga mkono
jitihada za Rais John Magufuli za kuleta
maendeleo kwa kulipa kodi bila shuruti ili
zipatikane fedha za kujenga miundombinu
kama barabara, reli, shule, madaraja,
hospitali na zahanati.
Kuhusu taarifa zilizozagaa kwenye
mitandao ya kijamii kwamba hata baadhi
ya mali za Kampuni ya Lugumi
zimeshikiliwa, Mkurugenzi huyo
alithibitisha kuwa habari hizo ni za kweli
ambapo wanashikilia nyumba za kifahari
za mfanyabiashara huyo.
“Mmeniuliza kwamba mmesikia nyumba
za Lugumi zimefungiwa ni kweli,
amefungiwa nyumba zake za kifahari na
anadaiwa Sh bilioni 14, yupo mtu anaitwa
Gm Dewji naye anadaiwa Sh bilioni 1.8,
Kampuni ya ujenzi ya Mutluhan
Construction anadaiwa Sh bilioni
45,”alisema.
Alisema wanaodaiwa wanapaswa kulipa
madeni yao TRA ndani ya siku 14 na
kwamba muda huo ukipita watapewa
maelekezo na serikali kama ni kuuza mali
hizo ili kufidia madeni yao.
Ofisa Mwandamizi wa TRA, ambaye
hakupenda jina lake litajwe alithibitisha
kwamba nyumba ya Lugumi iliyoko
Upanga mtaa wa Mazengo inashikiliwa na
mamlaka hiyo na ghorofa la kifahari
lililoko Mbweni JKT, Dar es Salaam.
“Hakuna siri maana mkienda kwenye hizo
nyumba mtakuta alama ambazo huwa
Yono wanaweka kwa nyumba
inayoshikiliwa, nendeni Upanga na kule
Mbweni JKT mtakuta hizo nyumba
tunazoshikilia,” alisema
Chanzo: HabariLeo
0 comments :
Post a Comment