Rais Magufuri kupokea taarifa la zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma. Soma zaid
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kesho
tarehe 28 Aprili 2017, atapokea Taarifa ya
zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi
wa Umma katika Ukumbi wa Chimwaga
Mkoani Dodoma.
Taarifa hiyo itawasilishwa kwa
Mheshimiwa Rais na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Mheshimiwa Angellah
Kairuki.
Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi
wa Umma liliendeshwa na Serikali kuanzia
Mwezi Oktoba mwaka 2016.
0 comments :
Post a Comment