Mauaji ya kutumia risasi yametokea wilayani Rufiji. Soma zaid
Mtu mmoja Aitwae Amri Chanjale (55),
mkazi wa kitongji cha Makaravati katika
Kijiji cha Umwe Kusini wilayani Rufiji
ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa
nyumbani kwake.
Tukio hilo limetokea jana saa 1.30 usiku
baada ya watu wasiojulikana kufika kwake
na kutekeleza shambulio hilo.
Marehemu huyo ambaye pia ni
mwanachama wa CCM ameuawa ikiwa ni
baada ya siku tano kuuawa kwa
Mohammed Malinda ambaye nae alikuwa
ni mwanachama wa chama hicho.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM
wilayani Rufiji, Musa Nyeresa
amethibitisha kuuawa kwa mwanachama
huyo kwa kupigwa risasi.chanzo jamii forums.
0 comments :
Post a Comment