Wakili Albert Msando ameomba kujiuzulu nafasi yake ya ushauri wa ACT.soma zaid
Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando
kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa
Chama chetu cha ACT Wazalendo.
Ndugu Msando anawajibika Kwani anapaswa,
nanukuu kutoka katika barua yake, "kuishi Kama
mfano Kwa jamii inayonizunguka".
Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi
mwenye mchango mkubwa katika chama katika
nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama.
Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa
kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni
matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi
katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza
na atakapohitajika kama mwanachama.
Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali
kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika
kujisahihisha kwake.
Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa
jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia
kupita katika mitihani iliyomkumba.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Dar es salaam
Mei 23, 2017
0 comments :
Post a Comment