Mwalimu wa sekondari ajiua kwa sumu aacha ujumbe huu.soma zaid
Mwalimu, Betson Sanga aliyekuwa
akifundisha Shule ya Sekondari Milundikwa
iliyopo wilayani Nkasi mkoani Rukwa amefariki
dunia baada ya kunywa sumu akiwa katika
nyumba ya kulala wageni mjini hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George
Kyando amesema kwamba mwalimu huyo alifariki
dunia juzi usiku huku akiwa ndani ya chumba
alichokuwa amepanga katika nyumba moja ya
kulala wageni iliyopo eneo la stendi kuu ya
mabasi yaendayo mikoani.
Kyando amesema chanzo cha kifo cha mwalimu
huyo bado hakijafahamika lakini aliacha ujumbe
mfupi wa maneno.
“Kama anadaiwa deni lolote na mtu amweleze
mkurugenzi ambaye ni mwajiri wake, lakini
asilaumiwe chochote juu ya kifo chake,"
amesema Kamanda Kyando wakati akinukuu
ujumbe huo wa marehemu.
Kamanda Kyando pia amesema uchunguzi wa
kitabibu umebainisha kuwa mwalimu huyo alijiua
kwa kunywa sumu.chanzo mwananch
0 comments :
Post a Comment