Rais Magufuli akutana na Boss wa ACACIA leo Ikulu kampuni imekubali kulipa deni lote wanalodaiwa na serikal.soma zaid
Rais John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya Canada Profesa John L. Thorton Ikulu jijini Dar es salaam. Kampuini Hiyo imemuahidi Rais Magufuli kulipa Deni lote wanalodaiwa na Tanzania, Katika mkutano huo, uliohudhuriwa na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Paramagamba Kabudi na Balozi wa Canada hapa nchini, Ian Myles umemalizika kwa mafanikio makubwa ambapo pande zote zimekubaliana kukaa meza moja kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali katika sekta ya madini.
0 comments :
Post a Comment