Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, June 14, 2017

Bunge lapigilia msumari dhidi ya hawa watu.soma zaid

Bunge limeitaka Serikali kuchukua hatua
kali dhidi ya wote watakaothibitika
kuhusika kuliingizia Taifa hasara na
kuwakosesha Watanzania fursa ya
kufaidika na rasilimali za madini.
Hoja hiyo imetolewa leo Jumatano
bungeni baada ya kamati iliyoundwa jana
na Spika Job Ndugai kupata maoni ya
namna Bunge linavyoweza kuunga mkono
juhudi binafsi zinazochukuliwa na Rais
John Magufuli kukabiliana na udanganyifu
unaofanywa kwenye sekta hiyo.
Kamati hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa
Newala Mjini, George Mkuchika baada ya
kukamilisha taratibu zote, imetoa
maazimio matatu ambayo yamepitishwa
na Bunge.
"Bunge linamuunga mkono Rais John
Magufuli na lipo tayari kutoa ushirikiano
wa dhati kadri itakavyohitajika kuhakikisha
juhudi hizi hazipotei bure na sekta ya
madini inachangia maendeleo ya
wananchi na Taifa kwa ujumla," amesema
Mkuchika.
Kukubaliana na kinachofanywa na Rais
Magufuli maazimio matatu yametolewa
ambayo ni kumpongeza na kuunga mkono
kwa hatua anazochukua, kumhakikishia
ushirikiano wakati wowote atakapohitaji
na kushauri kuchukuliwa kwa hatua kali
za kisheria kwa watakaobainika kushiriki
kulitia taifa hasara kutokana na
kuidhinisha mikataba mibovu na wizi
uliofanywa.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top