Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, June 14, 2017

Achoma moto nyumba baada ya mke wake kukataa kumfungulia mlango.soma zaid


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro
(ACP), Koka Moita, alisema mwenyekiti huyo
aliamua kuchukua mafuta ya petroli yaliyokuwa
kwenye pikipiki yake na kuichoma nyumba hiyo
kwa hasira kwa kile alichodai mkewe alionyesha
dharau.
“Kwa bahati nzuri hakuna vifo wala madhara kwa
binadamu yaliyotokea, lakini huyu Mwenyekiti
baada ya kufanya tukio hilo alifanikiwa kutoroka,
Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata katika Kijiji
cha Uswaa nje kidogo ya Kijiji cha Sawe akiwa
amejificha,” alisema Moita.
Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni ulevi
uliopindukia wa mtuhumiwa na wakati
anatekeleza kusudio lake alikuwa amelewa na
kumlalamikia mke wake kuwa alichelewa
kumfungulia mlango.
Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 6:00 usiku
katika Kijiji cha Sawe, Kata ya Masama
Mashariki, Tarafa ya Masama, Wilaya ya Hai.
Wakati huo huo, Shaban Juma, amefariki dunia
jana, baada ya kuangukiwa na mtungi wa zege
katika jengo la ghorofa 11 linalojengwa na
kumilikiwa na mfanyabiashara, Fredrick Shoo.
Mtungi huo ulianguka na kusababisha kifo, baada
waya ngumu inayotumika kupandishia mtungi huo
juu ya ghorofa kukatika katika ghorofa ya nane.
Jengo hilo refu kuliko yote katika mji wa Moshi,
linajengwa na Kampuni ya Wachina katika
Barabara ya Market Road.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top